Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luis Diaz, Bayern Munich mambo mazuri

DIAZ Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo kutoka Colombia, ambaye bado ana miaka miwili katika mkataba wake wa sasa, tayari ameonyesha nia ya kuondoka Anfield kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi na Bayern ndio inaonekana kudhamiria kumsajili.

LIVERPOOL, ENGLAND: MABOSI wa Liverpool wako tayari kulegeza msimamo wao kuhusu Luis Diaz na kukubali ofa ya chini ya Euro 80 milioni kutoka kwa Bayern Munich katika dirisha hili.

Mshambuliaji huyo kutoka Colombia, ambaye bado ana miaka miwili katika mkataba wake wa sasa, tayari ameonyesha nia ya kuondoka Anfield kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi na Bayern ndio inaonekana kudhamiria kumsajili.

Diaz, pamoja na Darwin Nunez, hawakujumuishwa kwenye kikosi cha mechi ya kirafiki ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya dhidi ya AC Milan katika ziara ya Asia iliyofanyika Jumamosi.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot, baadaye alithibitisha kuwa Diaz hakuwa sehemu ya timu kutokana na uvumi unaoendelea kuhusu mustakabali wake.

Kwa mujibu wa mwandishi Ben Jacobs, mabosi wa Liverpool wamekubali kwamba Diaz ataondoka katika dirisha hili na wako tayari kulegeza msimamo wao na kupokea ofa ya chini ya thamani yao ya awali ya Euro 80 milioni.

Hata hivyo, licha ya kuwa tayari kupunguza bei, staa huyu atajiunga na timu kwenda Tokyo kwa ajili ya sehemu inayofuata ya maandalizi yao ya msimu huko  Asia.

Bayern Munich inataka kuhakikisha inamsajili Diaz katika dirisha hili la usajili baada ya ofa yao ya awali ya Euro 68 milioni kukataliwa na mabingwa wa England.

Kikosi cha Arne Slot kinatarajiwa kurejea uwanjani Julai 30, kitakapoumana na Yokohama F. Marinos kwenye mechi nyingine ya kirafiki.

Hata hivyo, taarifa za ndani zinaeleza huenda Bayen ikakamilisha dili lake hivi karibuni na Diaz huenda asicheze tena hata kwenye mechi hizo za kirafiki.