Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lopez ‘alazimishwa’ kuwa shabiki Spurs

Muktasari:

  • Mwigizaji huyo alifanya kazi pamoja na mwimbaji na mwigizaji huyo maarufu wa Marekani katika mradi mpya uitwao Office Romance, na akatumia nafasi hiyo kujaribu kumvutia kuiunga mkono Spurs.

LONDON, ENGLAND: BRENTT Goldstein, nyota wa mfululizo wa michezo ya runinga ya Ted Lasso, amekiri katika mahojiano na TalkSPORT alikuwa akijaribu kumshawishi Jennifer Lopez kuwa shabiki wa Tottenham Hotspur, timu ambayo yeye mwenyewe anaishabikia.

Mwigizaji huyo alifanya kazi pamoja na mwimbaji na mwigizaji huyo maarufu wa Marekani katika mradi mpya uitwao Office Romance, na akatumia nafasi hiyo kujaribu kumvutia kuiunga mkono Spurs.

“Hana chaguo jingine,” alisema Goldstein kwa utani na kuongeza, pia alizungumzia msimu mgumu ambao Spurs imepitia uliokuwa wa kuumiza kihisia.

“Ulikuwa mbaya sana. Kuwa shabiki, hasa wa timu zetu ni kama kujiumiza mwenyewe. Ni jambo lenye maumivu. Lakini kupona na kuepuka kushuka daraja tulihisi kama kushinda Kombe la Dunia,” alisema mwingizaji huyo. Spurs iliponea kushuka Championship katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England msimu uliopita

Akimzungumzia straika wa zamani wa kikosi hicho anayekipiga Bayern Munich kwa sasa, Harry Kane, ambaye ana uhusiano mzuri naye alisema: “Ninavutiwa na kipaji chake, lakini zaidi ya yote ninavutiwa na moyo wake mkubwa nje ya uwanja. Nampenda Harry Kane. Siyo tu ni mmoja wa wanasoka bora kabisa tuliowahi kuwa nao, lakini kutokana na nilichokiona. Ni mtu mwenye roho safi. Hakuna kitu nachopenda zaidi kuliko mchezaji wa mpira mwenye moyo safi. Anaonekana kuwa mtu mwema kweli, na pia ni mchezaji wa kipekee. Ninafurahi sana kuwa naye katika filamu hii.”

Kwa upande wake, Jennifer Lopez pia alizungumzia ushiriki wake katika Office Romance akisema: “Lilikuwa tukio zuri sana. Wakati wa usomaji wa kwanza wa maandishi ya filamu mbele ya waigizaji wote, timu haikuwa na uhakika kama lingefanyiwa kazi vizuri, lakini kila mtu alianza kucheka kwa nguvu. Nikasema, ‘Mungu wangu, hili ni la kuchekesha sana,’ na tulifurahia sana wakati wa kurekodi tukio hilo.”

Ushirikiano huo kati ya Lopez, Brett na Kane katika Office Romance umeongeza hamasa kwa mashabiki wa filamu na soka, huku utani kuhusu kumgeuza Lopez kuwa shabiki wa Spurs ukiwa moja ya mambo yaliyovutia zaidi katika mahojiano hayo.