Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo amzidi Messi mara mbili

MAGWIJI Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa orodha hiyo, Ronaldo anapata takribani Pauni 187 milioni (Sh1.2 trilioni) kwa mwaka kupitia mkataba wake na Al-Nassr, huku mikataba ya matangazo na biashara ikimwingizia Pauni 37 milioni zaidi.

LONDON, ENGLAND: MSHAMBULIAJI mkongwe Cristiano Ronaldo ameendelea kutawala upande wa mapato katika soka la dunia, akimzidi mpinzani wake wa muda mrefu, Lionel Messi, kwa karibu mara mbili katika orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi duniani iliyotolewa na jarida la Forbes.

Nyota huyo wa Al-Nassr ya Saudi Arabia anakadiriwa kupata Pauni 225 milioni (Sh1.2 trilioni) kwa mwaka, kiasi kinachotokana na mshahara wake klabuni hapo pamoja na mikataba ya kibiashara.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, Ronaldo anapata takribani Pauni 187 milioni (Sh1.2 trilioni) kwa mwaka kupitia mkataba wake na Al-Nassr, huku mikataba ya matangazo na biashara ikimwingizia Pauni 37 milioni zaidi.

MAGWIJI

Mapato hayo yanakadiriwa kuwa sawa na Pauni 488,000 kwa siku, yakimuweka mbele ya Messi, anayekusanya takribani Pauni 108 milioni kwa mwaka.

Messi, anayeichezea Inter Miami ya Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), anakadiriwa kupata Pauni 52 milioni  kwa mwaka kupitia klabu hiyo, huku mikataba ya kibiashara ikimwongezea Pauni 56 milioni.

Ronaldo na Messi, ambao kwa zaidi ya muongo mmoja wamekuwa wakishindania nafasi ya kuwa mchezaji bora duniani, kwa pamoja wanachangia sehemu kubwa ya mapato ya wachezaji 10 wanaoongoza katika orodha hiyo, ambao kwa ujumla wanakadiriwa kuingiza Pauni 706 milioni kwa mwaka.

Katika nafasi ya tatu yupo mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe, anayekadiriwa kupata Pauni 75 milioni kwa mwaka baada ya kumaliza mkataba wake wa Pauni 15 milioni kwa mwaka na kampuni ya Nike.

MAGWI 02

Nafasi ya nne inashikiliwa na mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, anayekusanya takribani Pauni 64 milioni kwa mwaka. Mbali na mshahara wake, Haaland hunufaika na mikataba ya kibiashara na kampuni mbalimbali, zikiwamo Revolut na Nike.

Vinicius Junior wa Real Madrid anafunga tano bora kwa mapato ya Pauni 56 milioni kwa mwaka. Mshambuliaji huyo wa Brazil anadaiwa kunufaika na mkataba mpya na klabu hiyo unaomwingizia Pauni 25 milioni kwa msimu.

Kijana wa Barcelona, Lamine Yamal, anashika nafasi ya sita akiwa na mapato yanayokadiriwa kufikia Pauni 41 milioni kwa mwaka.

Yamal anapata sehemu kubwa ya fedha hizo kupitia mkataba wake na Barcelona, unaokadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 33.5 milioni kwa msimu, pamoja na mikataba ya kibiashara inayoongeza thamani yake nje ya uwanja.

Mchezaji huyo pia amevutia wadhamini kutokana na kukua kwa umaarufu wake, akiwamo kampuni ya mavazi ya American Eagle.

Akifuata ni mshambuliaji wa Al-Nassr na nyota wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane, anayekadiriwa kuingiza Pauni 40 milioni kwa mwaka.

Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham, anashika nafasi ya nane kwa mapato ya Pauni 34 milioni kwa mwaka.

Mbali na kipato chake uwanjani, Bellingham amekuwa akijijengea jina katika biashara kupitia mikataba na kampuni za Adidas, Louis Vuitton na Skims.

MAGWI 03

Nahodha wa England na mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane, anaingia katika orodha hiyo kwa mara ya kwanza, akishika nafasi ya tisa kwa mapato ya Pauni 32 milioni kwa mwaka.

Kane anakadiriwa kupata Pauni 400,000 kwa wiki kupitia mkataba wake na klabu hiyo ya Ujerumani, huku mikataba mingine ya kibiashara, ikiwamo na kampuni ya Skechers na huduma ya akili mnemba ya Google Gemini, ikichangia mapato yake.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Mohamed Salah, anafunga 10 bora kwa mapato ya Pauni 30 milioni kwa mwaka, baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na Trabzonspor unaomuingizia Pauni 363,000 kwa wiki.

Kuondoka kwa Salah Liverpool kunamaanisha kuwa Haaland ndiye mchezaji pekee wa Ligi Kuu England katika orodha hiyo.

Hata hivyo, kuingia kwa Bellingham na Kane kunafanya England kuwa na wachezaji wawili katika orodha hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013, walipokuwapo Wayne Rooney na David Beckham.

Mchezaji mkubwa aliyekosekana katika orodha hiyo ni mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema.

Benzema, ambaye ni mmoja wa washambuliaji mashuhuri wa kizazi chake, alikadiriwa kupata Pauni 78 milioni msimu uliopita kabla ya kuvunja mkataba wake na Al-Hilal. Kwa sasa hana klabu.