Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yashindwa kuamua kwa Samenyo, yabaki njia panda

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mabosi wa Liverpool wanaona wanaweza kutoa pesa nyingi ikiwa itawasilisha ofa Januari lakini ikishinda kuwasilisha wakati huo itakutana na ushindani mkubwa ifikapo mwisho wa msimu huu.

LIVERPOOL ipo kwenye wakati mgumu wa kufanya uamuzi kuhusu kuwasilisha ofa Bournemouth dirisha lijalo la majira ya baridi ya kiangazi kwa ajili ya Antoine Semenyo Januari, mwakani.

Mabosi wa Liverpool wanaona wanaweza kutoa pesa nyingi ikiwa itawasilisha ofa Januari lakini ikishinda kuwasilisha wakati huo itakutana na ushindani mkubwa ifikapo mwisho wa msimu huu.

Mbali ya wao, Man City pia imeonyesha nia ya kutaka kumsajili Semenyo, 25, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.

Kuingia kwa Man City katika dili hilo ndio kunaonekana kuichanganya Liverpool ambayo hapo awali ilionekana kuwa yenyewe katika mchakato huo.

Mabosi wa Bournemouth hawnaa haraka ya kutaka kumuuza staa huyu ambaye ni miongoni mwa wachezaji wao tegemeo wa kikosi cha kwanza akiwa amefunga mabao sita na kutoa asisti tatu,  katika mechi 12 za michuano yote.


Vinicius Jr

Mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Jr alikaribia kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika timu hiyo kabla ya kugoma na kuomba kuondoka.

Mkataba wa sasa wa staa huyu unamalizika mwaka 2027. Ameonyesha nia ya kuondoka kwa sababu haoni kama kocha Xabi Alonso anamwamini na anampa kipaumbele.

Tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa akikaa sana benchi na mechi kadhaa amekuwa akitolewa kabla ya mechi kumalizika.


Rodrigo Mendoza

MANCHESTER City imejiunga na Arsenal kufuatilia maendeleo ya kiungo wa Elche, Rodrigo Mendoza, 20, ambaye  Real Madrid pia imeonyesha kuvutiwa naye.

Staa huyu mwenye uwezo mkubwa wa kuchez kama kiungo wa katikati, amekuwa akitazamwa na maskauti wa vigogo wa Ulaya tangu mwaka jana.

Mkataba wa Mendoza na Elche unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Mabosi wa timu yake wanadaiwa kuhitaji zaidi ya Paun 40 milioni ili kumuuza.


Kalvin Phillips

LEEDS United imeulizia uwezekano wa kumsajili  kiungo wao wa zamani, Kalvin Phillips, 29, kwa mkopo kutoka Manchester City.

Hata hivyo, dili hilo halionekani rahisi kutokea kwani Phillips amewaambiwa wawakilishi wake anataka kujiunga na timu kutoka Ufaransa, Hispania na Ujerumani.

Staa huyu anataka kuondoka England kiujumla ili kujaribu changamoto sehemu nyingine akiamini anaweza kurudisha makali.


Andre Luiz 

Stoke City, Norwich City na Portsmouth wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya winga wa Rio Ave, Andre Luiz, 23, ambaye tayari anawindwa na klabu za  Ligi Kuu England ambazo ni pamoja na  Brentford na Sunderland.

Hata hivyo, klabu yake haiko tayari kumuuza winga huyo wa kimataifa wa Brazil katika dirisha lijalo badala yake inataka kuendelea kuwa naye hadi mwisho wa msimu.


Angelo Stiller

REAL Madrid imeanza mazungumzo na Stuttgart ya Ujerumani ili kumsajili kiungo wa timu hiyo, Angelo Stiller, 24, katika dirisha lijalo.

Madrid bado inapambana kutafuta viungo wenye umri mdogo ambao watakuwa na uwezo kama Toni Kroos na Luka Modric na kuiwezesha kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu. Ada ya uhamisho ya fundi huyu inatajwa kufikia Euro 30 milioni.


Givairo Read

MANCHESTER City huenda ikawasilisha ofa ya kumsajili beki wa kulia wa Feyenoord, Givairo Read, 19,  mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, huenda ikapigwa bao na Bayern Munich ambayo tayari imefanya mazungumzo na upande wa mchezaji. Mkataba wake na Feyenoord unamalizika mwaka 2027, na kuna uwezekano timu yake ikamuuza kwa Euro 35 milioni.


Gonzalo Garcia

REAL Madrid ipo tayari kusikiliza ofa ya kuanzia Euro 20 milioni kutoka kwa timu inayohitaji mshambuliaji wao chipukizi Gonzalo Garcia, 21, ambaye anawindwa na timu nyingi za England ikiwamo Sunderland, Aston Villa na Wolves.

Garcia amekuwa miongoni mwa vijana waliowahi kutabiriwa kuwa hazina ya baadaye lakini amekuwa hapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.