Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yamvizia Rayan wa Bournemouth

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Liverpool inaweza kulipa kitita cha Pauni 130 milioni ili kumpata nyota huyo wa Brazil, iwapo itaamua kutumia kipengele cha kuvunja mkataba wake ambacho kitaanza kutumika mwaka 2027.

LIVERPOOL inatajwa kuwa tayari kuvunja rekodi yake ya usajili ili kumnasa mshambuliaji wa Bournemouth, Rayan, 20, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Liverpool inaweza kulipa kitita cha Pauni 130 milioni ili kumpata nyota huyo wa Brazil, iwapo itaamua kutumia kipengele cha kuvunja mkataba wake ambacho kitaanza kutumika mwaka 2027.

Rayan amekuwa akivutia kutokana na uwezo wake wa kushambulia, jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa na Liverpool kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kwa muda mrefu.

Iwapo Liverpool italipa kiasi hicho, usajili huo utakuwa miongoni mwa gharama kubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo na unaweza kuvunja rekodi yake ya sasa ya usajili.

Hata hivyo, bado hakuna uthibitisho kwamba Liverpool imefikia makubaliano ya kumnunua Rayan, huku suala la kifungu hicho cha Pauni 130 milioni likitarajiwa kuwa muhimu katika mazungumzo yoyote yatakayofanyika.

Msimu huu amecheza mechi nne za Ligi Kuu England ingawa hajafunga bao bao hata moja na kuna uwezekano mkubwa akaondoka dirisha dogo la usajili la Januari endapo Liverpool itakuwa na ushawishi mkubwa kifedha.


Florian Wirtz

Bayern Munich imeanza kufuatilia kwa karibu hali ya kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Florian Wirtz, anayekipiga Liverpool. Wirtz (23), anaendelea kuwa mchezaji muhimu Liverpool, lakini Bayern imeelezwa kuwa inafuatilia kwa karibu maendeleo yake na huenda ikajaribu kumsajili iwapo nafasi itapatikana.


Ronald Araujo

Liverpool imepewa nafasi ya kumsajili moja kwa moja beki wa kimataifa wa Uruguay, Ronald Araujo, 27, baada ya kukamilika kwa muda wa mkopo wake kutoka Barcelona. Liverpool ina kipengele cha kumnunua Araujo kwa ada ya Euro 55 milioni, sawa iwapo itaamua kuendelea naye baada ya kumalizika kwa mkataba wa mkopo.



Pierre Kalulu

Juventus haiko tayari kumuuza beki wake wa kimataifa wa Ufaransa, Pierre Kalulu, dirisha la usajili la Januari, licha ya kutakiwa na Manchester United na Liverpool. Kalulu, 26, amehusishwa na uwezekano wa kuhamia moja kati ya klabu hizo mbili za Ligi Kuu England, lakini Juventus imeweka wazi haina mpango wa kumuachia.


Jadon Sancho

Kocha wa Borussia Dortmund, Niko Kovac, amesema klabu hiyo haina mpango wa kumsajili tena winga wake wa zamani, Jadon Sancho, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru. Sancho, 26, aliwahi kung’ara Dortmund kabla ya kuhamia Manchester United, lakini sasa mustakabali wake umekuwa gumzo baada ya kuachwa bila klabu.


Louis Page

Borussia Dortmund imejiunga na Manchester United kuwania saini ya kiungo wa Leicester City, Louis Page huku klabu hiyo ya Ujerumani ikituma maskauti kumfuatilia kwa karibu kinda huyo mwenye umri wa miaka 18. Page, raia wa England, ameibua shauku ya klabu hizo mbili zinazomfuatilia kwa lengo la kumsajili katika siku zijazo.


Luke Chambers

Klabu kadhaa za Championship pamoja na Celtic zimeanza kuonyesha nia ya kumsajili beki wa Liverpool na timu za vijana za England, Luke Chambers, katika dirisha la usajili la Januari. Chambers, mwenye umri wa miaka 22, anatajwa kuwa kwenye rada za klabu hizo zinazotazamia kumnasa katika dirisha lijalo.


Arda Guler

Real Madrid imempa kiungo wake kinda, Arda Guler, mkataba wa miaka sita, katika hatua inayolenga kuendelea kumweka kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo. Guler(21), ni raia wa Uturuki na amekuwa akivutia hisia za makocha mbalimbali.


Giorgio Scalvini

Newcastle United imepata pigo katika kumsajili beki wa Atalanta, Giorgio Scalvini, baada ya kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu yake. Scalvini (22), alikuwa akifuatiliwa na Newcastle, lakini kusaini mkataba huo kunaifanya klabu hiyo kukabiliwa na kazi kubwa zaidi ikiwa itataka kumng’oa kutoka Atalanta.


Martin Zubimendi

Kiungo wa Arsenal, Martin Zubimendi, huenda akalazimika kufikiria kuondoka katika klabu hiyo dirisha la usajili la Januari baada ya kupoteza nafasi yake kikosi cha kwanza. Zubimendi, 27, amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuondoka Arsenal, huku Chelsea na Real Madrid zikitajwa miongoni mwa zinazomfuatilia kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania.