Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viktor Gyökeres hatarini ‘kupigwa bei’ Arsenal

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kocha wa timu hiyo Mikel Arteta alikuwa amemwamini Kai Havertz katika michezo minne ya mwanzo ya msimu huu, lakini hatimaye alimpa Viktor Gyökeres nafasi ya kuanza katika mchezo dhidi ya Napoli uliochezwa Naples juzi lakini bado staa huyo wa zamani wa Sporting Lisbon alishindwa kuonyesha makali yake.

TAARIFA zimeanza kuzangaa kuwa Arsenal ipo mbioni kumuuza mshambuliaji wake Viktor Gyökeres kwenye usajili wa dirisha kubwa mwakani.

Kocha wa timu hiyo Mikel Arteta alikuwa amemwamini Kai Havertz katika michezo minne ya mwanzo ya msimu huu, lakini hatimaye alimpa Viktor Gyökeres nafasi ya kuanza katika mchezo dhidi ya Napoli uliochezwa Naples juzi lakini bado staa huyo wa zamani wa Sporting Lisbon alishindwa kuonyesha makali yake.

Mshambuliaji huyo alionekana kutokuwa na ushawishi mkubwa katika mchezo huo. Lakini kwa kiasi kikubwa ni vigumu kumlaumu, kutokana na namna Napoli walivyocheza kwa kujilinda kwa kina ndani ya nusu yao ya uwanja.

Hali hiyo inazua swali iwapo Arteta alipaswa kuendelea kumtumia Havertz katika nafasi ya mshambuliaji, hasa baada ya Mjerumani huyo kuonyesha kiwango bora katika ushindi dhidi ya Chelsea mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Arsenal na uongozi wa staa huyo watakaa baadaye mwezi ujao kujadiliana kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo kwenye kikosi cha Arsenal na kama hatakuwa na uhakika wa kucheza basi Arsenal wanalazimika kumuuza.

Timu mbalimbali zimekuwa zikimwania staa huyo raia wa Sweden akiwemo Barcelona ya Hispania pamoja na Inter Milan ya Italia, ambazo zilimtaka hata kabla hajatua London


LEWIS HALL

Newcastle United bado inaweza kumuuza beki wake wa kushoto, Lewis Hall, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuripotiwa kukubaliana kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo hadi mwaka 2031.

Hall, ambaye ni raia wa England, hivi karibuni alihusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United.


LISANDRO MARTINEZ

Manchester United iko tayari kumpa Lisandro Martinez mkataba mpya wa muda mrefu endapo beki huyo wa kati wa Argentina ataepuka majeraha na kufanya vizuri katika msimu wa 2026/27 huko Old Trafford.

Martinez ana miaka 28 na amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.


YASIN AYARI

Brighton ina matumaini makubwa ya kufikia makubaliano ya mkataba mpya na kiungo wa Sweden, Yasin Ayari.

Mazungumzo yanaendelea vizuri na pande zote zinaaminika kuwa karibu kukamilisha dili hilo kiungo huyo mwenye miaka 22 amekuwa akionyesha kiwango cha juu sana kwa siku za hivi karibuni.


KAORU MITOMA

Mustakabali wa Kaoru Mitoma huko Brighton bado haujawa na uhakika.

Winga huyo wa Japan, mwenye miaka 29, hana uwezekano mkubwa wa kuongeza mkataba wake ambao unamalizika mwakani, jambo linaloweza kumfanya aondoke klabuni hapo mapema kwenye dirisha la usajili la Januari huku akiwa anawindwa na timu kadhaa kubwa kutokana na ubora wake uwanjani.


MANU KONE

Baada ya kushindwa kumsajili Manu Kone katika dirisha la majira ya kiangazi, Chelsea inaweza kurejea kwa kiungo huyo wa AS Roma kwenye dirisha la Januari.

Dili hilo linaweza pia kumhusisha winga wa England, Jamie Gittens, ambaye anaweza kuhamia AS Roma katika mpango wa kubadilishana wachezaji.

Kone ana miaka 25, huku Gittens akiwa na miaka 22.


ALEXIS MAC ALLISTER

Liverpool ina mpango wa kumsajili kiungo mwingine katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani.

Hatua hiyo inaweza kumfanya kiungo wa Argentina, Alexis Mac Allister, kushuka zaidi kwenye orodha ya wachezaji wanaopewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Anfield au timu hiyo ikipata dili zuri inaweza kumuachia aondoke akapate changamoto nyingine nje ya Anfield. Mac Allister ana miaka 27.


ALEX BAENA

Atletico Madrid haina mpango wa kumuuza kiungo wa Hispania, Alex Baena, kwa sasa licha ya kuwepo kwa ofa nono kutoka Manchester City ya England.

Baena, mwenye miaka 25, bado anaonekana kuwa sehemu muhimu ya mipango ya Atletico kuelekea michezo ya msimu  huu ambao timu hiyo inapambana kuhakikisha kuwa inafanya vizuri.


NICOLO TRESOLDI

Manchester United na Tottenham Hotspur zilipeleka wawakilishi nchini Ubelgiji Jumanne kumtazama mshambuliaji wa Club Brugge, Nicolo Tresoldi.

Mjerumani huyo mwenye miaka 22 anaendelea kuvutia macho ya vigogo hao wawili wa Ligi Kuu England baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu msimu uliopita.


DAVID ALABA

Beki wa Austria, David Alaba, anaweza kuibukia Mexico baada ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Club America.

Alaba, mwenye miaka 34, aliondoka Real Madrid katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi na sasa anaweza kuanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka nchini Mexico, beki huyo mwenye kiwango cha hali ya juu amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kubwa ikiwemo Arsenal.


MALICK THIAW

Klabu za Liverpool na Manchester United zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya beki wa kimataifa wa Ujerumani, Malick Thiaw, ambaye kwa sasa anakipiga Newcastle United.

Thiaw, mwenye umri wa miaka 25, amevutia macho ya vigogo hao wa Ligi Kuu England kutokana na uwezo wake katika eneo la ulinzi. Hata hivyo, Newcastle United haina mpango wa kumuuza beki huyo kwa sasa.