Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gabriel Martinelli hashikiki Saudia

MARTINELI Pict

Muktasari:

  • Martinelli amefunga mabao yake katika dakika ya 18, 43 na 50, huku Ollie Watkins akifunga mawili katika dakika ya tisa na 53.

RIYADHI, SAUDI ARABIA: GABRIEL Martinelli ameanza kuonyesha makali yake katika Ligi Kuu ya Saudi Arabia, baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja na kuiongoza Al Hilal kuichapa Al Taawoun mabao 6-0, mchezo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa  Al Taawoun.

Martinelli amefunga mabao yake katika dakika ya 18, 43 na 50, huku Ollie Watkins akifunga mawili katika dakika ya tisa na 53.

Sultan Mandash alikamilisha ushindi huo kwa kufunga bao la sita dakika ya 75.

Watkins ndiye aliyeanza kuifungulia Al Hilal mlango wa mabao dakika ya tisa, kabla Martinelli kuongeza bao la pili dakika ya 18.

MART 01

Martinelli aliendelea kuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Al Taawoun na kuongeza bao lake la pili dakika ya 43, akiipeleka Al Hilal mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0.

Dakika tano tu baada ya kipindi cha pili kuanza, Martinelli alifunga bao lake la tatu na kukamilisha mabao matatu katika mchezo huo.

Watkins ameongezabao lake la pili dakika ya 53 kabla ya Mandash kufunga bao la sita dakika ya 75 na kukamilisha ushindi mkubwa wa Al Hilal.

MART 02

Huo ulikuwa mchezo wa tatu kwa Martinelli tangu alipojiunga na Al Hilal akitokea Arsenal, huku kiwango chake kikianza kuwapa matumaini mashabiki wa klabu hiyo kuhusu mchango wake katika msimu huu.

Watkins naye ameendelea kuonyesha uwezo mkubwa tangu alipojiunga na Al Hilal, huku ushirikiano wake na Martinelli ukiipa timu hiyo nguvu zaidi katika safu ya ushambuliaji.

Ushindi huo umeipa Al Hilal nguvu katika mbio za kuwania ubingwa wa Saudi Arabia na kuonyesha kuwa usajili wa wachezaji hao wapya unaanza kuleta matokeo chanya.

Kwa Martinelli, mabao hayo matatu yamekuwa mwanzo mzuri wa maisha yake Saudi Arabia na kuongeza matarajio kwamba anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika harakati za Al Hilal kutwaa mataji msimu huu.