Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yaamua kujisubirisha kwa Marc Guehi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Liverpool haitaki kupambana na dili hilo Januari kutokana na bei kubwa inayoweza kuwekwa na Crystal Palace katika ada ya kumruhusu kuondoka katika kikosi hicho.

LIVERPOOL imeamua kusubiri hadi wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwakani kabla ya kuanza tena mazungumzo ya kumsajili beki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 25.

Liverpool haitaki kupambana na dili hilo Januari kutokana na bei kubwa inayoweza kuwekwa na Crystal Palace katika ada ya kumruhusu kuondoka katika kikosi hicho.

Guehi anaendelea kuwa chaguo la kwanza kwa Liverpool katika mipango ya timu hiyo ya muda mrefu ya kuimarisha safu ya ulinzi ambayo ina idadi kubwa ya wachezaji tegemeo wanaoweza kuondoka ndani ya misimu miwili ijayo.

Mchezaji huyo ambaye pia anawindwa na Real Madrid na pamoja na Bayern Munich alikuwa karibu kujiunga na Liverpool katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu, lakini dili hilo lilifeli kwenye dakika za mwisho baada ya kocha wa timu yake kusitisha mpango huo.

Guiehi ambaye pia ni nahodha wa Crystal Palace ameshawaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anataka kuondoka mwakani ama katika dirisha la Januari au mwisho wa msimu.

Tangu kuanza kwa msimu huu, mchezaji huyo ambaye alizaliwa Ivory Coast, lakini anaichezea timu ya taifa ya England, amecheza mechi 28 za michuano yote inayoshirikia timu hiyo akiwa amefunga mabao matatu na kutoa asisti nne.



Conor Gallagher

ATLETICO Madrid inatarajiwa kuachana na kiungo wa timu ya taifa ya England, Conor Gallagher, 25, katika dirisha la usajili la Januari.

Manchester United, Tottenham Hotspur na Newcastle United zote zimeonyesha nia ya kumsajili staa huyo katika dirisha hilo.

Mabosi wa Atletico wanahitaji zaidi ya Pauni 40 milioni kwa ajili ya kumuuza nyota huyo ambaye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka.


Robert Lewandowski

CHICAGO Fire ya Ligi Kuu Marekani  ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski, 37.

Hata hivyo, inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Fenerbahce ya Uturuki na klabu kadhaa za Saudi Arabia.

Lewandowski ni miongoni mwa wachezaji wenye mvuto mkubwa sokoni baada ya kuelezwa Barca haina mpango kuendelea naye.


Scott McTominay

MANCHESTER United inatajwa kuwa na  mpango wa kumrudisha kiungo wa Napoli na timu ya taifa ya Scotland, Scott McTominay, 29, katika viunga vya Old Trafford.

McTominay aliondoka United kutafuta changamoto mpya na muda mwingi wa kucheza, lakini sasa benchi la ufundi la timu hiyo limevutiwa naye na linataka kumrudisha ili kuboresha eneo la kiungo. Hata hivyo, dili hilo linaweza kuwa gumu.


Joshua Zirkzee

EVERTON imepanga kutuma maombi ya usajili wa mkopo kwa nyota wa Manchester United, kiungo wa England, Kobbie Mainoo, 20, na mshambuliaji wa  kimataifa wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, 24.

Uongozi wa Everton unaamini wachezaji hao wataongeza nguvu na ushindani kikosini katika nusu ya pili ya msimu. Manchester United bado inafanya tathmini juu yao.


Marcos Senesi

BARCELONA inapanga kumsajili beki wa Bournemouth na timu ya taifa ya Argentina, Marcos Senesi, 28, kwa uhamisho huru katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mabosi wa Barca wanaona Senesi ni chaguo sahihi la kuimarisha safu ya ulinzi na pia atapatikana bure.

Mkataba wa Senesi na Bournemouth unamalizika mwishoni mwa msimu na hakuna mazungumzo kumsainisha dili jipya.


Abdul Fatawu

BOURNEMOUTH imejiunga rasmi kwenye vita ya kumsajili winga wa Leicester City na timu ya taifa ya Ghana, Abdul Fatawu, 21.

Fatawu amewahi kuhusishwa na Crystal Palace, Everton na Sunderland ambazo zote zinadaiwa kuwa bado zinahitaji kumsajili katika dirisha lijalo.

Leicester City haijaweka wazi msimamo wake wa kumuuza, lakini taarifa zinaonyesha huenda ikawa tayari kufanya hivyo ikiwa itawasilishwa ofa nono.


Brennan Johnson

BOUNEMOUTH inataka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Wales, Brennan Johnson, 24.

Mabosi wa Bournemouth wanamwangalia Brennan kama mmoja kati ya wachezaji wanaoweza kuziba pengo la mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Antoine Semenyo, 25, ambaye kuna uwezekano akaondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi ambapo timu kibao zimeonyesha nia ya kumsajili.