Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Roma abonga na Zirkzee, Man Utd mh!

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa fundi huyu amefanya mazungumzo na kocha wa Roma, Gian Piero Gasperini ambaye ndio amemhakikishia suala hilo ikiwa ni sehemu ya kumshawishi akubali kujiunga nao.

STRAIKA wa Manchester United, Joshua Zirkzee, 24, amehakikishiwa kuwa atapewa nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha AS Roma ikiwa atakubali kujiunga nao katika dirisha la majira ya baridi mwakani.

Inaelezwa fundi huyu amefanya mazungumzo na kocha wa Roma, Gian Piero Gasperini ambaye ndio amemhakikishia suala hilo ikiwa ni sehemu ya kumshawishi akubali kujiunga nao.

Zirkzee amekuwa akihitaji kuondoka Man United tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu kwa sababu hapati nafasi ya kutosha hali inayomweka katika hatihati ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kitakachoshiriki Kombe la Dunia mwakani.

Awali, ilielezwa kwamba Man United ilikuwa tayari kumwachia katika dirisha lijalo, lakini sasa imesitisha kwa sababu ya majeraha ambayo yanawaandama katika kikosi pamoja na kukosekana kwa wachezaji wao walioenda AFCON, Bryan Mbeumo na Amad Diallo.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na msimu huu amecheza mechi 11 za michuano yote na kufunga bao moja.


Manuel Ugarte

MANCHESTER United imepanga kusikiliza ofa zitakazowasilishwa kwa ajili ya kiungo wao wa kimataifa wa  Uruguay, Manuel Ugarte, 24, katika dirisha la usajili la Januari.

Ugarte alijiunga na United huku mashabiki wa timu hiyo wakiwa na matarajio makubwa juu yake, lakini bado hajafanikiwa kujijengea nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza kutokana na ushindani mkali uliopo katika eneo la kiungo.

Mkataba wake na United unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Santiago Castro

NOTTINGHAM Forest, Chelsea na Aston Villa zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Bologna na timu ya taifa ya Argentina Santiago Castro, 21.

Staa huyu amezivutia sana timu hizi kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 21 za michuano yote.


Lewis Dunk

BEKI wa kati wa Brighton na timu ya taifa ya  England, Lewis Dunk mwenye umri wa miaka 34, amekubali kuendelea kusalia katika kikosi cha kwanza cha Brighton kwa msimu mmoja zaidi baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Awali, iliripotiwa kwamba fundi huyu anaweza akaondoka Januari mwakani. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 16 za michuano yote. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Micky van de Ven

TOTTENHAM Hotspur ipo tayari kumpandisha maslahi na kumpa mkataba mpya beki wake wa kimataifa wa Uholanzi, Micky van de Ven, mwenye umri wa miaka 24.

Spurs inataka kumpa staa huyu mshahara mnono na kumsainisha mkataba mpya ili kuzuia asiondoke katika dirisha lijalo ambapo timu nyingi barani Ulaya zimeonyesha nia ya kuwasilisha ofa ili kumsajili.

Van de Ven amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Spurs kutokana na kasi, nguvu na uwezo wa kuzuia mashambulizi ya kushtukiza.


Manu Kone

KIUNGO wa AS Roma na timu ya taifa ya Ufaransa, Manu Kone, 24, anatarajiwa kujiunga na Manchester United katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza kuwa pande zote zimefikia makubaliano ya awali, huku United ikimwangalia Kone kama chaguo sahihi la kuimarisha safu yao ya kiungo.

Mkataba wa sasa wa Kone unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Kacheza mechi 21.


James McAtee

CHELSEA na Leeds United ni kati ya klabu za Ligi Kuu England zinazofuatilia kwa karibu maendeleo ya kiungo wa Manchester City, James McAtee, mwenye umri wa miaka 23, anayecheza kwa mkopo Nottingham Forest.

McAtee, aliyekulia katika akademi ya Manchester City, amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha Forest, hali inayosababisha baadhi ya timu kutaka kuwasilisha ofa ya kuvunja mkataba wake.


Davide Bartesaghi

ARSENAL inataka kufanya jaribio la kumsajili beki wa kushoto wa AC Milan, Davide Bartesaghi, raia wa Italia mwenye umri wa miaka 19.

Bartesaghi ambaye ni miongoni mwa wachezaji vijana wanaofanya vizuri Italia kwa sasa ameonyesha nia ya kutimka na alikuwa akifuatiliwa na maskauti wa Arsenal kwa muda mrefu.

Mabosi wa Milan wanadaiwa kuwa wapo tayari kumuuza ikiwa wataridhishwa na ofa itakayowasilishwa mezani.