Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool, Tottenham macho kodo kwa Camavinga

Muktasari:

  • Ripoti zinaeleza kuwa kiungo huyo wa Ufaransa anataka kupata changamoto sehemu nyingine na anaamini atarudi katika ubora ikiwa atafanya hivyo.

KIUNGO wa Real Madrid na Ufaransa, Eduardo Camavinga, 23, ambaye hajaitwa katika kikosi cha timu ya taifa hilo kitakachoshiriki Kombe la Dunia, anadaiwa kuwa tayari kuondoka  dirisha lijalo la kiangazi.

Ripoti zinaeleza kuwa kiungo huyo wa Ufaransa anataka kupata changamoto sehemu nyingine na anaamini atarudi katika ubora ikiwa atafanya hivyo.

Miongoni mwa klabu zinazohitaji kumsajili ni pamoja na Tottenham Hotspur na Liverpool ambazo bado hazijaanza rasmi mazungumzo. Camavinga ameendelea kuwa mchezaji muhimu katika mfumo wa Real Madrid kutokana na uwezo wa kucheza nafasi nyingi katika eneo la kiungo, lakini shida  amekuwa hana nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza ambapo mara nyingi huingia akitokea benchi na mara chache huanza dakika 90. Mkataba wake Real Madrid unatarajiwa kumalizika 2029 na msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote.


Denzel Dumfries

BEKI wa Inter Milan, Denzel Dumfries, 30, anaweza kuondoka Julai, mwaka huu ikiwa timu inayomtaka italipa Euro 25 milioni. Inaelezwa kiasi hicho cha pesa kiliwekwa katika  moja ya vipengele vya mkataba wake na Inter. Beki huyo wa kulia wa Uholanzi amekuwa mchezaji muhimu Inter kwa zaidi ya misimu miwili na klabu nyingi zilikuwa zikimuwinda tangu mwaka jana. Uwepo wa kipengele hicho, unadaiwa kuzivutia timu nyingi.


Anthony Gordon

NEWCASTLE United imesisitiza kwamba inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 75 milioni kwa ajili ya kummuuza winga wa kimataifa wa England, Anthony Gordon, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Gordon anawindwa na Bayern Munich ambayo imekuwa ikiomba kupunguziwa bei hadi kufikia Pauni 60 milioni. Staa huyo ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu Newcastle hali iliyosababisha Bayern kuvutiwa naye. Mkataba unaisha 2030.


Federico Valverde

KIUNGO wa Real Madrid, Federico Valverde, 27, anaripotiwa kuwa na mpango wa kuendelea kubaki licha ya tetesi zinazodai timu kibao Ulaya zinahitaji saini yake. Man City, Man United na PSG ni miongoni mwa klabu zinazodaiwa kuanza mazungumzo na wawakilishi wake. Moja ya sababu zilizodaiwa kuchangia Valverde kuripotiwa kuwa anaweza akaondoka ni kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya wachezaji Real Madrid


Mateus Fernandes

PSG ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kiungo wa West Ham United na timu ya taifa ya Ureno,  Mateus Fernandes, 21, na huenda ikatuma ofa ili kumsajili katika dirisha lijalo. Hata hivyo, Fernandes anataka kusubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kufanya uamuzi wowote kwani anataka kuona ikiwa West Ham itabaki Ligi Kuu England au itashuka daraja. Mbali ya PSG, huduma yake inahitajika na Man United na Liverpool.


Matias Soule

ASTON Villa inapanga kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Matias Soule , 23, kutoka AS Roma katika dirisha lijalo. Ripoti zinaeleza mpango wa Soule kutua Villa umejumuishwa katika dili la winga wa Uholanzi, Donyell Malen, 27,ambaye msimu huu amecheza kwa mkopo Roma akitokea Villa. Inaelezwa Roma imevutiwa na Malen na inataka kumsainisha mkataba, hivyo Soule anaweza kutumika kama sehemu ya ofa.


Mike Maignan

CHELSEA imemuweka katika rada kipa wa AC Milan na timu ya taifa ya Ufaransa, Mike Maignan, 30, kutoka AC Milan kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hata hivyo, matumaini ya Chelsea kumpata yanaweza kuathiriwa ikiwa haitafanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Maignan anachukuliwa mmoja wa makipa bora Ulaya kwa sasa na mkataba anamaliza 2031.


Michael Kayode

BEKI kisiki wa Brentford, Michael Kayode, 21, amesisitiza kuwa ameridhika na maisha ndani ya kikosi licha ya klabu kadhaa ikiwemo Juventus kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. Beki huyo raia wa Italia ameendelea kuvutia vigogo Ulaya kutokana na uwezo wake wa kukaba. Mkataba wa sasa wa Kayode unatarajiwa kumalizika 2032 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote.