Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool tatu za kibabe zinakuja!

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Kocha wa miamba hiyo, Arne Slot tayari ameshawanasa Jeremie Frimpong, Milos Kerkez, Hugo Ekitike na Florian Wirtz kuongeza nguvu kwenye kikosi chake cha kibingwa na sasa kinapiga hesabu za kumnasa straika wa Newcastle, Alexander Isak na beki wa kati wa Crystal Palace, Marc Guehi.

LIVERPOOL, ENGLAND: PENGINE ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, lakini hilo wala haliifanyi Liverpool kubweteka. Miamba hiyo ya Anfield imekuwa bize sana kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, ikijaribu kunasa vifaa vya maana ili kutetea taji lao la ligi msimu ujao na kufanya vizuri michuano ya Ulaya.

Kocha wa miamba hiyo, Arne Slot tayari ameshawanasa Jeremie Frimpong, Milos Kerkez, Hugo Ekitike na Florian Wirtz kuongeza nguvu kwenye kikosi chake cha kibingwa na sasa kinapiga hesabu za kumnasa straika wa Newcastle, Alexander Isak na beki wa kati wa Crystal Palace, Marc Guehi.

Kama Slot atafanikiwa kuwanasa wachezaji wote anaowataka, basi ataweza kutumia fomesheni tatu tofauti zitakazoifanya Liverpool kuwa moto uwanjani.

1. Mabeki watatu wa kati (3-4-3)

Msimu uliopita ilitumia sana fomesheni hii, lakini kwa usajili wa msimu huu mtindo huo wa kutumia safu ya ulinzi ya mabeki watatu wa kati, itakuwa na moto msimu huu, endapo itafanikiwa kumpata Guehi, ambaye atakuja kuungana na Ibrahima Konate na Virgil van Dijk kwenye kumlinda kipa Alisson.

Hilo litawafanya Frimpong na Kerkez kwenda mbele kushambulia wakicheza wing-backs, wakicheza kwenye mstari sawa na viungo wa kati, Alexis Mac Allister na Ryan Gravenberch. Na kwenye safu ya wakali watatu wa mbele, kutakuwa na Wirtz, Mohamed Salah na Isak atakayeongoza mashambulizi.

2.Kurejesha mtindo wa 4-3-3

Wanasema kama haijavunjika, usilazimike kuirekebisha na hicho ndicho unachoweza kusema kuhusu matumizi ya fomesheni ya 4-3-3 kwenye kikosi cha Liverpool. Kocha Slot anaweza kuendelea kutumia fomesheni hiyo, akiwatumia mchezaji Conor Bradley akipewa nafasi ya kuanza mbele ya Frimpong, huku Konate na Van Dijk wakiendelea kuwa pacha kwenye beki ya kati. Hii itamfanya Dominik Szoboszlai kupata nafasi kwenye safu ya kiungo akiwa mmoja wa viungo watatu kwenye eneo hilo, huku katika eneo la ushambuliaji kutakuwa na Salah, Wirtz na Isak.

3.Wirtz kucheza kati kwenye 4-2-3-1

Mtindo mwingine wa uchezaji ambao Slot anaweza kuutumia ni kujaribu kumtumia Wirtz kwenye Namba 10, ili kutumia fomesheni ya 4-2-3-1. Hapo, Guehi atacheza pacha na Van Dijk kwenye beki ya kati na Robertson atacheza beki ya kushoto, huku golini atakuwa Giorgi Mamardashvili. Kwenye Namba 10, atacheza kiungo ghali, Wirtz, huku upande mmoja akicheza Ekitike na mwingine Salah na Isak ataongoza mashambulizi.