Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool, Isak ngoma tamu, Newcastle Utd yatia ngumu

TETESI Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa Liverpool inazungumza na Newcastle kuhusu ada ya uhamisho inayotajwa kufikia Pauni 150 milioni.

STRAIKA wa Newcastle United, Alexander Isak, 25, amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na majogoo wa Liverpool ambapo atasaini mkataba wa miaka mitano na kupokea mshahara unaotajwa kufikia Pauni 300,000 kwa wiki.

Kwa sasa Liverpool inazungumza na Newcastle kuhusu ada ya uhamisho inayotajwa kufikia Pauni 150 milioni.

Liverpool haitaki kulipa kiasi hicho cha pesa na badala yake inafanya mazungumzo ili kupunguziwa. Mkataba wa staa huyu wa kimataifa wa Sweden, unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Isak ambaye hajasafiri na Newcastle kwenda Singapore kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, ameripotiwa kuwajulisha mabosi wa timu hiyo kwamba anataka kuondoka katika dirisha hili, pia hatosaini mkataba mpya ambao wamemwekea mezani hivi karibuni.

Newcastle ambayo haionekai kabisa kutaka kumuuza staa huyu ilimweke ofa ya mkataba mpya ambao ulikuwa na mshahara wa takribani Pauni 250,000 kwa wiki lakini Isak alikataa.

Kocha wa Newcastle Eddie Howe anatamani kumwona mchezaji huyu akicheza sambamba na Anthony Elanga ambaye amejiunga nao hivi karibuni akitokea Notthingham Forest.

Liverpool ambayo katika dirisha hili imeshafanikisha usajili wa washambuliaji kadhaa ikiwemo Hugo Ekitike kutika Entrach Frankfurt bado inataka kuboresha zaidi eneo lao la  ushambuliaji ili kuhakikisha inatetea taji lao kwa msimu ujao.

Isak ambaye pia ana uraia wa Eritrea alikuwa katika mipango ya majogoo hawa wa Jiji la Liverpool tangu dirisha lililopita la majira ya baridi lakini ilishindikana kwa ssbabu Newcastle haitaki kuona akiondoka.


Jack Grealish

EVERTON imeingia kwenye vita dhidi ya Napoli na West Ham United kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo wa Manchester City na England, Jack Grealish, 29, katika dirisha hili la usajili kwa mkopo wa msimu mmoja. Mpango huo wa kumchukua kwa mkopo unaonekana kuzingatiwa kwa asilimia ndogo na mabosi wa Man City ambao wanahitaji kumuuza mchezaji huyo moja kwa moja.

‎Grealish ni miongoni mwa mastaa ambao kocha Pep Guardiola amewapa ruhusa ya kuondoka kwa sababu hawapo katika mipango yake kuelekea msimu ujao.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Yoane Wissa

MABOSI wa Brentford wanadaiwa kuwa hawataki kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo, Yoane Wissa, kwenda Newcastle United katika dirisha hili kwa gharama yoyote hadi pale watakapokuwa na uhakika wa kupata mbadala wake. Wissa, 26, anawindwa na Newcastle kwa sababu inamwona kuwa mbadala sahihi kwenda kuboresha eneo la ushambiliaji ikiwa Alexander Isak ataenda Liverpool.


Jorrel Hato

CHELSEA ipo katika hatua za mwisho kufanikisha dili linalodaiwa kuwa na thamani ya Euro 40 milioni kwenda Ajax kwa ajili ya kumsajili beki kisiki wa timu hiyo na Uholanzi, Jorrel Hato, 19, katika dirisha hili. Hato ambaye amekuwa katika rada za Chelsea kabla hata ya kuanza michuano ya Kombe la Dunia la Klabu iliyofanyika Marekani na Chelsea kuwa bingwa.


Morten Hjulmand

MANCHESTER United imewasilisha ofa ya Euro 40 milioni kwenda Sporting Lisbon kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo wa klabu hiyo na Denmark, Morten Hjulmand katika dirisha hili. Hata hivyo, taarifa zimefichua kuwa ofa hiyo imekataliwa kwa sababu Sporting inataka Euro 50 milioni. Staa huyo, 26, mbali ya Man United, saini yake pia inahitajiwa na Juventus


Dan Ndoye

WAWAKILISHI wa Nottingham Forest wanaripotiwa kuwasili Italia kufanya mazungumzo na Bologna ili kuipata saini ya staa wa  klabu hiyo na timu ya taifa ya Uswisi, Dan Ndoye, katika dirisha hili. Ndoye, 24 anaripotiwa kuwaambia mabosi wa Bologna hataki kucheza Serie A kwa msimu ujao na badala yake anataka kutua England.


Adama Traore

NOTTINGHAM Forest inafanya mpango wa kumsajili winga wa Fulham na Hispania, Adama Traore, 29, ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na kocha Nuno Espirito Santo walipokuwa Wolves. Traore anadaiwa kuwa ni pendekezo la Nuno ambaye anaamini atasaida katika eneo la ushambuliaji. Mabosi wa Fulham hawapo tayari kumuachia.


Igor Paixao

MPANGO wa Leeds kutaka kumsajili winga wa Feyenoord, Igor Paixao, 25, katika dirisha hili la majira ya kiangazi unadaiwa kufeli baada ya kufichuliwa kuwa mshambuliaji huyo yupo katika hatua nzuri ya kujiunga na Marseille katika dirisha hili. Winga huyo wa kimataifa wa Brazil amevutiwa sana na ofa ya Marseille kwa sababu mbali ya kumpa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya pia inampa pesa nyingi.