Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool ilivyompiga mtu bao sita ugenini

Muktasari:

  • Liverpool imeshajihakikishia kufurahia Krismasi ikiwa kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya Chelsea kubanwa na kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Everton.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imezidi kujitanua kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kushusha kipigo cha mabao 6-3 dhidi ya Tottenham Hotspur, katika mechi kali kabisa ya michuano hiyo iliyofanyika kabla ya Krismasi.

Liverpool imeshajihakikishia kufurahia Krismasi ikiwa kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya Chelsea kubanwa na kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Everton.

Lakini, kikosi hicho cha kocha Arne Slot kiliangusha kipigo kizito kwa Spurs na kudhihirisha kwamba Liverpool kwa sasa ni timu iliyo kwenye kiwango bora kabisa cha soka lake duniani. Luis Diaz alifunga bao la kuongoza kwa Liverpool na lile la sita, Mohamed Salah alifunga mara mbili na kuasisti mara mbili na mabao ya Dominik Szoboszlai na Alexis Mac Allister yalionyesha kiwango bora kabisa kwa vijana hao wa Slot.

Spurs yenyewe ilifunga mabao yake kupitia kwa James Maddison kabla ya mapumziko, huku mawili ya kipindi cha pili yalifungwa na Dejan Kulusevski na Dominic Solanke. Kwa kiwango hicho cha Liverpool, kinawafanya wapewe nafasi kubwa ya kunyakua taji lao la kwanza la Ligi Kuu England tangu mwaka 2020, ambapo litakuwa taji lao la pili la ligi kwenye karne hii ya 21. Katika kipute hicho cha Spurs na Liverpool kuna takwimu 11 matata kabisa.

– Trent Alexander-Arnold alitengeneza bao la kwanza la Liverpool kwa pasi matata kabisa. Hiyo ina maana asilimia 27 ya mabao ya Alexander-Arnold kwenye Ligi Kuu England yametokea kwenye mechi dhidi za Big Six.

– Alexander-Arnold ametengeneza nafasi nne dhidi ya Spurs, nyingi kuliko mchezaji yeyote aliyekuwa uwanjani kwenye mchezo huo. Nafasi zote nne hazikuwa za mipira ya kutenga na mbili kati ya hizo, zilikuwa nafasi kubwa kabisa za mashambulizi.

– Bao la Diaz ina maana Spurs imeruhusu kufungwa wa kwanza kwenye mechi 14 tofauti ilizocheza nyumbani kwenye Ligi Kuu England mwaka huu 2024; mara nyingi zaidi ndani ya mwaka mmoja katika michuano hiyo (Kama ilivyokuwa kwa Crystal Palace mwa 2017, Ipswich na Spurs mwaka 1994).

– Spurs sasa imeruhusu mabao 7 katika dakika 15 za kipindi cha kwanza, ni Ipswich Town (8) na Southampton (8) ndizo zilizoruhusu mabao mengi zaidi kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

– Mohamed Salah ni mchezaji wa kwanza kwenye historia ya Ligi Kuu England kufunga 10+ na kuasisti 10+ katika kipindi cha misimu minne mfululizo kwenye Ligi Kuu England.

– Kwa misimu sita, Mo Salah amefunga na kuasisti kwa zaidi ya 10+; ikiwa ni zaidi ya mchezaji mwingine yeyote kwenye Ligi Kuu England, akimzidi Wayne Rooney, ambaye alifunga zaidi ya mabao 10 na kuasisti zaidi ya mabao 10 katika kipindi cha misimu mitano mfululizo.

– Na Mo Salah amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha idadi ya tarakimu mbili kwenye kufunga na kuasisti ndani ya msimu mmoja wa Ligi Kuu England kabla ya kufika Krismasi.

– Mo Salah ameweka rekodi pia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuchangia mabao 32 kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ikiwa ni zaidi ya mabao 10 kwa mchezaji anayemfuatia kwa karibuni, Bukayo Saka.

– Liverpool inakuwa timu ya pili kufunga mabao sita kwenye Ligi Kuu England kwenye mechi ya ugenini dhidi ya Tottenham Hotspur baada ya Chelsea mwaka 1997.

– Liverpool itakuwa kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakati wa Siku ya Krismasi ikiwa ni mara yao ya saba kwenye Ligi Kuu England baada ya 1996, 2008, 2013, 2018, 2019 na 2020.

– Tottenham mechi zao tatu za mwisho ilizocheza nyumbani kwenye michuano yote imeshuhudia mabao 23, huku tisa yakifungwa kwenye mechi hiyo ya Jumapili baada ya mabao sita kwenye mechi ya Chelsea na mabao saba dhidi ya Manchester United katika Kombe la Ligi.