Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lionel Messi atatua huku

MESSI Pict

Muktasari:

  • Messi alikuwa Inter Miami tangu 2023 na ameshinda Kombe la Ligi pamoja na Supporters’ Shield akiwa na timu hiyo ya Florida, Marekani.

FLORIDA, MAREKANI: HATIMA  ya Lionel Messi katika soka baada ya kuondoka Inter Miami imeanza kufanyiwa kazi na wawakilishi wake, taarifa zikieleza mazungumzo kuhusu timu anayojiunga nayo yameshaanza.

Messi alikuwa Inter Miami tangu 2023 na ameshinda Kombe la Ligi pamoja na Supporters’ Shield akiwa na timu hiyo ya Florida, Marekani.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina ana tuzo za Ballon d’Or nane - ya mwisho akiipata mwaka jana na anachukuliwa na wengi kuwa mchezaji bora wa muda wote katika historia.

Messi alipitia kwenye kituo maarufu cha kukuza vipaji cha La Masia, Barcelona na alicheza mechi ya kwanza ya kikosi cha wakubwa 2004.

Akiwa Camp Nou alishinda mataji 10 La Liga, manne Ligi ya Mabingwa Ulaya,  matatu Uefa Super Cup, matatu Kombe la Dunia la Klabu, saba Copa del Rey na mataji saba Supercopa.

Messi alifunga mabao 672 katika mechi 778 akiwa na Barcelona kabla ya kuhamia Paris Saint-Germain 2021 hadi 2023 alikofunga 32 katika mechi 75 na kushinda mataji mawili ya Ligue 1, kabla ya kujiunga na Inter Miami.Me-ssi amefunga mabao 49 katika mechi 59 akiwa na Inter Miami, na mkataba wake na timu hiyo ya MLS unamalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Hivyo, kuna shaka kuhusu hatima yake baada ya mwaka huu kuisha na taarifa zinaeleza ipo timu iliyowahi kuwa na nia ya kumsajili ambayo sasa huenda ikarejea tena kwa ajili ya kumchukua.

Kwa mujibu wa tovuti ya  Teamtalk, Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF), umefungua tena mazungumzo na wawakilishi wa Messi kwa lengo la kumshawishi kujiunga na Ligi Kuu Saudi Arabia.

Nchi hiyo ilikuwa miongoni mwa machaguo ya Messi alipoondoka PSG 2023, kabla hajageuka na kwenda Marekani, lakini sasa unaonekana kuwapo kwa uwezekano wa uhamisho kwenda huko.

Nia ya Saudi Arabia inatokana na azma ya kumfanya Messi pamoja na mpinzani wake wa muda mrefu, Cristiano Ronaldo, kuwa sura za Ligi Kuu ya nchi hiyo (Saudi Pro League).

Taarifa zinaeleza: “Kwa sasa Messi anaendelea na Inter Miami akiwa amejikita kikamilifu kwenye majukumu yake ya MLS na Kombe la Dunia la Klabu akiwa na timu yake ya sasa. Lakini Mfuko wa Uwekezaji wa Saudi Arabia una azma ya kujaribu tena - safari hii ukitarajia matokeo tofauti.”

“Klabu ambayo Messi ataweza kujiunga nayo katika Ligi Kuu Saudi Arabia bado haijatajwa na mabosi wa ligi hiyo wanataka kwanza kujua kama atakuwa tayari au la.

“Baada tu ya Messi kuonyesha utayari wa uhamisho ndipo mabosi wataanza kutathmini ni ipi kati ya klabu nne ambazo ni Al Ahli, Al Hilal, Al Ittihad au Al Nassr  itakuwa chaguo sahihi kwake. Lakini hilo litajadiliwa katika hatua ya baadaye, si kwa sasa.”