Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lijendi kasema...hawatoboi

Muktasari:

  • Chelsea ambayo ilibeba Kombe la Dunia la Klabu la FIFA, fainali zilizofanyika Marekani mwezi uliopita, haikufanya vizuri sana katika Ligi Kuu England msimu uliopita ingawa ilimaliza katika nafasi ya nne na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: LEJENDI wa Liverpool, Jamie Carragher amesema licha ya kutumia Pauni 250 milioni katika usajili wa dirisha hili, haioni Chelsea ikichukua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao.

Chelsea ambayo ilibeba Kombe la Dunia la Klabu la FIFA, fainali zilizofanyika Marekani mwezi uliopita, haikufanya vizuri sana katika Ligi Kuu England msimu uliopita ingawa ilimaliza katika nafasi ya nne na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Carragher alisema haoni kama wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo dirisha hili wataongeza chochote, akisisitiza usajili wa klabu hiyo umekuwa hauna athari kubwa licha ya uwepo wa wachezaji wengi.

"Nikiitazama Chelsea, nawaza kuhusu ilichofanya kwenye Kombe la Dunia la Klabu, kila mtu alitaka kulishinda," alisema beki huyo wa zamani wa Liverpool kwenye kipindi cha The Overlap Fan Debate.

"Real Madrid ilitaka sana kulishinda, PSG vivyo hivyo na Manchester City pia, timu zote ambazo tunazichukulia ni miongoni mwa timu bora kabisa. Kwa hiyo naamini ushindi huo ni jambo kubwa na utasaidia kujenga uhusiano kati ya Kocha Enzo Maresca na mashabiki, kitu ambacho hakikuwepo msimu uliopita."

"Lakini sina hakika kama utaipeleka Chelsea karibu na ubingwa. Kwa miaka ya karibuni, Chelsea imefanya usajili ambao unaonekana kama wachezaji wengi wanabadilika bila kuongezeka kwa ubora wa kikosi.

"Najua Cole Palmer amekuwa wa kipekee, lakini maeneo mengine, uwezo wa wachezaji karibia wote unafanana, mfano halisi ni Jamie Gittens kasajiliwa kisha Noni Madueke kaondoka, hakuna ongezeko la ubora na hilo naliona kwenye nafasi nyingi Chelsea."

Dirisha hili ni kama ilivyozoeleka kwenye madirisha mengine ya usajili miaka ya hivi karibuni, hushuhudiwa wachezaji wakubwa kadhaa wakiondoka Stamford Bridge ikiwa ni sehemu ya kufanya mabadiliko.

Hadi sasa mastaa ambao wameshauzwa ni pamoja na Joao Felix, Kepa Arrizabalaga na Kiernan Dewsbury-Hall ambao jumla imepatikana Pauni 150 milioni katika mauzo yao.

Wachezaji wapya walioingia ni pamoja na Joao Pedro (Pauni 60 milioni), Liam Delap (Pauni 30 milioni), Jorrel Hato (Pauni 37 milioni), Estevao Willian (Pauni 28 milioni), Dario Essugo (Pauni 18.5 milioni), na Mamadou Sarr (Pauni 12 milioni).

Carragher, ambaye awali amewahi kuikosoa Chelsea kwa kutoa mikataba ya muda mrefu kupita kiasi, anaamini katika kikosi cha matajiri hao Cole Palmer ni moja kati ya wachezaji bora lakini amezungukwa na wachezaji ambao sio levo yake.

"Anaweza kuwa kama Steven Gerrard katika timu ambayo haitoshi kiushindani, jambo linalokatisha tamaa."

Chelsea itaanza msimu wa 2025-26 Agosti 17 kwa mechi ya London Derby dhidi ya Crystal Palace kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.