Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yawekeza mabilioni kujenga kikosi

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Wakati wengine wakitangaza wachezaji walioachana nao na wengine wakianza rasmi kambi, Azam FC imejiamulia kuanza kwa kutangaza wachezaji wao wapya.

Msimu wa 2026/27 inatarajiwa kuanza katikati ya Agosti na timu kadhaa zimeshaanza maandalizi ya msimu mpya.

Wakati wengine wakitangaza wachezaji walioachana nao na wengine wakianza rasmi kambi, Azam FC imejiamulia kuanza kwa kutangaza wachezaji wao wapya.

PUM 04

KIPRE JR

Amerejea nyumbani baada ya kuondoka mwaka 2024 akitimkia MC Alger ya Algeria.

Azam FC imetumia zaidi ya shilingi bilioni moja kumrejesha.

Ada ya uhamisho ambayo wamelipa kwa MC Alger ni Euro laki mbili na thelathini elfu ambazo ni takribani shilingi za Tanzania milioni mia saba.

Hiki ndicho kiasi ambacho MC Alger walikitoa kumnunua Kipre Jr.

Kwa hiyo Azam FC ni kama wamewarudishia tu pesa yao.

Hata hivyo, Kipre mwenyewe amelipwa dola laki mbili kama ada ya kusainia mkataba.

Hii ni sawa na shilingi milioni mia tano za Tanzania.

Ada ya uhamisho na ada ya kusainia mkataba unafanya jumla ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili.

PUM 03

HENRI STANIC

Beki wa kati raia wa Ubelgiji kutoka klabu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Wazazi wake wana asili ya Afrika; baba ni mtogo na mama ni mkongo wa DRC.

Ametokea klabu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini na alitaka kurudi Ulaya ambako alikuwa akicheza kabla ya kuja Afrika.

Lakini Azam FC ikapambana kwa ushawishi wa nguvu ya pesa hadi akashuka Chamazi.

Ada ya uhamisho kwa Stellenbosch ni dola laki mbili na nusu, ambazo ni takribani shilingi za Tanzania milioni mia sita.

Yeye mwenyewe amelipwa dola laki tatu, sawa na takribani shilingi za Tanzania milioni mia saba hamsini.

Ada ya uhamisho kwenda Stellenbosch na ada ya kusainia mkataba kwenda kwa mchezaji mwenyewe zinafanya jumla ya shilingi bilioni moja na milioni mia tatu.

PUM 02

LUPINI MAWUKU DIEUMERCI

Kitasa cha klabu ya Maniema ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kama kuna wachezaji wagumu kuwapata basi ni wa kutoka nchi hii...hasa klabu ya Maniema.

Waulize Yanga...Maxi Nzengeli anaenda msimu wa tatu huu akiwa kwa mkopo kutoka Maniema.

Jephte Kitambala ameondoka Azam FC baada ya mkopo wake kuisha na mazungumzo ya kuendeleza naye kushindikana kutokana na ugumu uliowekwa na Maniema.

Kwa kifupi ni kwamba klabu hiyo inayomilikiwa na Gabriel Amisi Kumba maarufu kama Tango Four, ni ngumu sana kufanya nayo biashara.

Huyu jamaa ni Jenerali wa jeshi akiongoza kikosi cha ardhini kamandi ya nane huko Kivu Kaskazini.

Awali alikuwa mwenyekiti wa AS Vita, na ndiye aliyemleta Ibenge Afrika kutoka China.

Akakorofishana na AS Vita ndipo akaanzisha klabu yake ya Maniema.

Wachezaji wake huwasainisha mikataba mirefu, hadi miaka mitano.

Sasa ukimtaka, atakupa kwa mkopo ambao utaulipia mwaka mmoja mmoja...au zaidi kama una msuli wa pesa.

Na hata ukitaka kumnunua moja kwa moja...hela yako tu, lakini jasho itakutoka.

Kitambala kwa mfano, Azam FC ilimchukua kwa mkopo wa mwaka mmoja kwa dola laki moja na nusu...zaidi ya shilingi milioni mia tatu.

Baada ya mkopo kuisha, Azam FC wakataka kumnunua moja kwa moj, sio tena mkopo.

Lakini Maniema wakaweka ada kubwa ya dola laki saba kumnunua moja kwa moja au ule mkopo wa dola laki moja na nusu uendelee.

Azam ikakaa vyote...ikamrudisha Kitambala na kumtaka Lupini...roho yao kwenye safu ya ulinzi, inshu ikawa inshu...jamaa wakakaza hasa.

Azam FC ikawatoka dola laki nne kumnunua moja kwa moja, sio mkopo.

Hii ni sawa na shilingi bilioni moja za Tanzania.

Yeye mwenyewe amelipwa dola laki moja, sawa na shilingi milioni mia mbili na hamsini za Tanzania.

Gharama za jumla ni shilingi bilioni moja na milioni mia mbili na hamsini.

PUM 01

ENOCK MOLIA

Raia mwingine wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka klabu ya FC Lupopo.

Winga mwenye kasi maarifa na shabaha ya magoli.

Pia anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati au kiungo mshambuliaji.

Yeye ndiye mchezaji pekee anayecheza ligi ya nyumbani ambaye taifa lilimlilia awepo kwenye kikosi cha Kombe la Dunia.

Ila kocha Sebastian Desabre hakufungua masikio...akamuacha.

Kumpata Molia, Azam FC ilibidi itoe dola laki nne na kuzima ndoto za Yanga ambayo iliweka dola laki mbili.

Pesa hizo ni sawa na shilingi za Tanzania bilioni moja.

Molia mwenyewe amelipwa dola laki mbili na nusu, sawa na takribani shilingi milioni.

Kwa kifupi Molia ameigharimu Azam FC zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu.

PUM 05

HASSAN MUBIRU

Winga wa klabu ya Villa ya Uganda. Huyu hajagharimu pesa kubwa kama hao wengine.

Ada ya uhamisho wake ni dola lakini moja na ishirini, sawa na takribani shilingi za Tanzania milioni tatu.

Na yeye mwenyewe alipewa dola elfu hamsini...sawa na takribani shilingi za Tanzania milioni mia moja na thelathini.

Gharama ya jumla ni zaidi ya shilingi milioni mia nne.

Japo gharama yake sio kubwa kwa kulinganisha na wale wengine, lakini ana kastori ka kipekee kidogo.

Wakati anasaini Azam FC, kuna timu kutoka Ulaya Mashariki ilianza kumfukuzia.

Waliposikia amesaini Azam, wakapeleka ifanya dola laki tatu ili wamnunue....yaani Azam imuuze hata kabla haijamtumia.

Hapo ndipo Azam ikabaini kwamba kumbe wameokotoa dodo.


PESA NDEFU

Kwa jumla Azam FC imewekeza zaidi ya bilioni tano na milioni mia tano kwa wachezaji hawa tu ambao imeshawatambulisha hadi sasa.

Na hapo bado gharama zingine ndogo ndogo kama ada ya wakala ambayo kimsingi huwa haipungui asilimia kumi ya ada ya uhamisho.

Gharama za tiketi za ndege na hoteli wachezaji kuja kusaini na kuondoka.

Gharama zingine ambao huwa haziandikwi hasa kwa ajili ya ushawishi...kama yale mambo ya fulani mpe kiasi fulani ili akalainishe mambo sehemu fulani.


WANA HAKI WAFIKIRIE KUHAMA LIGI

Sasa kwa uwekezaji kama huu halafu timu inakosa ushindi kwa sababu tu ya makosa ya upande mmoja ya waamuzi, lazima roho ziwaume.

Wanaona bora waende Zanzibar ambako gharama za kucheza ligi sio kubwa. Uwanja ni aidha Amaan au Gombani, basi.

Hakuna safari ndefu ya Kigoma, Bukoba wala Mbeya.

Yawezekana Azam FC hawana mpango wa kuhama, lakini ni hasira zilizotokana na maumivu ya kukosa haki.

Hata Yanga na Simba zimewahi kutoa hizi kauli.

Yanga waliutaka kuhamia Zambia, na Simba wakataka kuhamia Burundi.

Kwa hiyo Azam FC kusema watahamia Zanzibar sio kauli mpya sana.

Isitoshe Zanzibar ni Bado Tanzania...na hata sasa ligi ya Bara inachezwa katika viwanja vya huko.