Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lamine: Mbappe na mimi ndo bora zaidi duniani

LAMINE Pict

Muktasari:

  • Baada ya siku kadhaa za vipande vya mahojiano vilivyokuwa vikitolewa kabla ya wakati, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amefunguka kuhusu masuala ambayo hakuwahi kuyazungumzia hadharani mara nyingi kuanzia haiba na nafasi yake katika Kombe la Dunia hadi tuzo ya Ballon d’Or na uzoefu wake kuhusu ubaguzi wa rangi.

BARCELONA, HISPANIA: MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lamine Yamal  amezungumzia kuhusu masuala mbalimbali ikiwamo tuzo ya mchezaji bora Ulaya maarufu kama Ballon d’Or akisema, “mwaka huu ningestahili kushinda kutokana na kile nilichoshinda.”

Yamal amesema hayo katika mahojiano yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu na kipindi cha Movistar cha Universo Valdano ambayo hatimaye yametolewa.

Baada ya siku kadhaa za vipande vya mahojiano vilivyokuwa vikitolewa kabla ya wakati, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amefunguka kuhusu masuala ambayo hakuwahi kuyazungumzia hadharani mara nyingi kuanzia haiba na nafasi yake katika Kombe la Dunia hadi tuzo ya Ballon d’Or na uzoefu wake kuhusu ubaguzi wa rangi.


LAMI 01

MAPENZI YA SOKA

Katika hili, Yamal anasema: “Watu wananitilia shaka zaidi kwa sababu ya hilo. Kwamba kwa sababu tayari nimeshinda vitu vingi, sitaki kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mara tu niliposhinda Kombe la Dunia (2026), nilitaka kulishinda tena. Ninaishi kwa ajili ya soka na kupitia soka.”


LAMI 05

MAFANIKIO YA AJABU

Mchezaji huyo pia amegusia suala la mafanikio yake na kupanda kwa kasi katika kilele cha soka la ushindani duniania akifananishwa na mastaa wakongwe waliomtangulia.

“Tumekuwa na nyota wakubwa kama Leo (Messi) na Cristiano (Ronaldo), lakini sidhani kama tumewahi kuona wachezaji wengi wakishinda vitu vingi mapema hivi katika maisha yao ya soka hadi sasa. Watu wanafikiri kwamba kwa sababu nimeshinda vitu, nitapumzika. Lakini bado nina mambo mengi ya kufikia katika historia ya soka.”


LAMI 02

HAIBA YAKE

Juu ya haiba ya mchezo huo, Yamal anasema: “Najidai kwa mengi. Kabla ya kwenda Euro (2024) nilifikiri haitakuwa vigumu sana kushinda. Kabla ya Kombe la Dunia (2026) nilikuwa na mawazo kwamba tutashinda. Kila mara nafikiri tutamfunga (Real) Madrid. Msukumo huo mara nyingi ni kitu chanya (kuhusu maisha ya soka).”

Hata hivyo, kuhusu watu wanavyomfikiria, nyota huyo anasema: “Kwangu mimi ni kama msisimko. Siwezi kucheza mechi bila watu kutarajia kitu kutoka kwangu. Kwa hiyo ni kitu ambacho soka pekee ndilo linanipa.”

“Nilipokuwa mtoto sikuwahi kuhisi kuwa nilikuwa bora zaidi katika timu yangu. Kila mara niliwaona wengine na kufikiri kwamba nilipaswa kufanya zaidi. Wakati fulani, nilipopandishwa daraja, niligundua kwamba nilikuwa tofauti na wengine. Lakini kila mara najaribu kuboresha (kiwango) kwa sababu nina mambo elfu ambayo bado nayakosa.” Yamal pia amezungumzia alivyocheza katika Kombe la Dunia 2026 ambako kuna wakati hakuwa katika ubora wa juu zaidi, akijifichia kwenye mafanikio ya wengine.

LAMI 06

“Sikufurahi baada ya kushinda Kombe la Dunia. Jeraha halihusiani na hilo. Ingawa nilifanya mambo mengi ambayo watu hawakuyaona, sikuridhika na nilichokifanya mwenyewe. Najua mchezaji mwingine ambaye angekuwa na kiwango nilichokuwa nacho angekuwa na Kombe bora la Dunia, lakini mimi ningeweza kufanya zaidi. Nina hamu ya kushiriki kombe lijalo,” anasema.

Hata hivyo, katika suala la kutofanikiwa anaamini ni kwa sababu ya roho mbaya, akisema: “Naamini kuwa na roho mbaya inayodhibitiwa vizuri ni jambo zuri. Lakini iwe inadhibitiwa. Kwa sababu inasaidia timu nzima. Kila mara nataka wachezaji wenzangu wanaofikiri kuwa wao ni bora zaidi.”

Na katika suala la nafasi yake uwanjani, Yamal anatia neno, “sijui nitaishia kucheza katika nafasi gani, lakini nitakuwa mshambuliaji kila wakati. Hata hivyo, hamtaniona Lamine mwenye miaka 16 akiwa ameganda pembeni mwa uwanja. Kidogo kidogo, kadiri ninavyokaribia eneo la hatari, ndivyo nitakavyokuwa hatari zaidi.”


LAMI 03

MPINZANI WAKE, TUZO BALLON D’OR

Mchezaji huyo aliulizwa juu ya mpinzani ajaye baada ya Messi na Ronaldo kuanza kuaga katika soka la ushindani.

“Jambo moja kuhusu mimi ni kwamba nimepitia hatua za ukomavu kwa haraka sana. Tayari nimezoea zaidi ya inavyotarajiwa. Kuna mechi ambazo nafikiri ningekuwa huru zaidi. Niko mtulivu kwa sababu najua ninaweza kutoa zaidi. Ni vigumu sana kumpata mtu anayesema yuko katika kiwango changu,” anasema.

Vilevile dogo amepita katika tuzo zijazo za Ballon d’or akisema kwamba kila kitu kipo freshi mara tu mambo yatakapokamilika na kwamba, ushindi utakuwa njiani kwenye masiha yake na wenzake.

Anasema: “Tuzo hii sasa inatathminiwa kwa namna tofauti. Messi na Cristiano walipokuwapo, kila mtu alijua kwamba walikuwa bora zaidi, hivyo hakukuwa na mjadala. Tatizo ni kwamba watu wanahukumu mambo ambayo siyo vigezo vya Ballon d’Or, kama kusema kwamba inapaswa kupewa mchezaji wa PSG kwa sababu alishinda Ligi ya Mabingwa (Ulaya).

“Tuzo hiyo inapaswa kupewa mchezaji bora zaidi duniani, basi. Siyo kwa mchezaji aliyefunga mabao 80 kwa sababu unapofunga mabao mengi kiasi hicho unapata Pichichi (tuzo ya mfungaji bora LaLaiga kwa msimu). Hivyo ni vitu viwili tofauti ambavyo watu hawavielewi. Mchezaji bora zaidi duniani ni yule ambaye unafurahia kumtazama wakati wa mechi, mchezaji ambaye ni tofauti na wengine wote. Tuzo hii itakaporejea kuangazia nilichoeleza, itarejesha thamani ambayo imekuwa nayo kihistoria.”


LAMI 04

UNGEMPA NANI TUZO?

Katika swali na nani iwapo Yamal anhekuwa jaji au mpigakura wa tuzo hiyo angeitoa kwa nani, anajibu huku akitabasamu, lakini akiwa na jibu zito.

“Anayestahili ni mchezaji bora zaidi duniani. Nani hasa atapata tuzo hiyo ni mjadala mrefu. Kwa dhati naamini kuna wachezaji wawili bora zaidi duniani. Na mwaka huu ningestahili kushinda kutokana na kile nilichoshinda (ubingwa wa Dunia na Laliga). Mbappe na mimi ndiyo wachezaji bora zaidi duniani. Kila anayetazama mechi anajua hilo. Tuna ushindani wa moja kwa moja na nimemshinda katika kila kitu. Amefunga mabao mengi, lakini ndiyo maana alishinda Pichichi,” anasema Yamal.

Na kuhusu Kombe la Dunia iwapo linapaswa kuamua kuhusu Ballon d’or, nyota huyo anasema kuna mambo ya kuzingatia na ni muhimu.

“Hata mimi sioni hilo kuwa sahihi. Sidhani kama shindano moja linapaswa kuamua tuzo hiyo. Lakini bahati ni kwamba mimi niko katika timu ya taifa iliyoshinda Kombe la Dunia. Kama England ingeshinda, bado ningesema Mbappe na mimi ndiyo wachezaji bora zaidi,” anasema akimzungumzia Mbappe ambaye ni mpinzani wake pia katika LaLiga.