Kwa nini Kuminga kaichagua Wolves badala ya Lakers?
Muktasari:
- Kuminga amefikia mwisho moja ya sakata iliyodumu muda mrefu zaidi katika kipindi hiki cha usajili wa NBA, ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ameamua kuichagua Timberwolves, huku akiripotiwa kukubaliana na mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Dola 12.4 milioni, ukiwa na kipengele kinachomruhusu kuamua kuhusu msimu wa pili baada ya ule wa kwanza kumalizika.
LOS ANGELES, MAREKANI: NYOTA wa kikapu Jonathan Kuminga anaripotiwa kuichagua Minnesota Timberwolves badala ya Lakers, hatua iliyoiweka Los Angeles katika hali ya kukosa mmoja wa wachezaji muhimu iliokuwa ikiwalenga zaidi katika nafasi ya forward.
Kuminga amefikia mwisho moja ya sakata iliyodumu muda mrefu zaidi katika kipindi hiki cha usajili wa NBA, ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ameamua kuichagua Timberwolves, huku akiripotiwa kukubaliana na mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Dola 12.4 milioni, ukiwa na kipengele kinachomruhusu kuamua kuhusu msimu wa pili baada ya ule wa kwanza kumalizika.
Muundo huo wa mkataba unampa Kuminga nafasi ambayo amekuwa akiitafuta kwa muda mrefu katika maisha yake; kudhibiti mustakabali wake.
Baada ya kukosa mikataba yenye thamani kubwa zaidi katika mazungumzo yaliyopita, Kuminga atapata nafasi nyingine ya kujithibitisha kabla ya uwezekano wa kurejea kwenye soko la wachezaji huru msimu ujao. Akiwa na msimu mzuri Minnesota, alirejea sokoni akiwa na nafasi ya kupata mkataba bora wa muda mrefu ambao ameshindwa kuupata. Kwa Wolves, Kuminga anajaza pengo lililo wazi kufuatia kuondoka kwa Julius Randle akitarajiwa kuwa na jukumu muhimu sambamba na LaMelo Ball, Anthony Edwards, Jaden McDaniels na Rudy Gobert, huku timu hiyo ikijaribu kuunda upya kikosi chake kumzunguka Edwards.
Hata hivyo, uamuzi wake una athari pia kwa timu nyingine, kwani Los Angeles Lakers ilikuwa miongoni mwa timu zilizotajwa mara kwa mara kama sehemu inayoweza kumsajili forward huyo, na inaripotiwa iliendelea kuwa kwenye mbio za kumsajili hadi mwisho. Badala yake, imejikuta ikikosa mchezaji ambaye angeweza kusaidia kuziba moja ya upungufu wake mkubwa katika kikosi.
Hata hivyo, anaingia katika kipindi muhimu cha maisha yake ya kikazi kwa sababu dili lake linaweza kuwa ambalo huenda lisiwe na mslahi bora mbele ya safari iwapo hataonyesha ubora, na hasa kwa kuwa timu aliyotua huenda isimyumie ipasavyo. Maswali kuhusu nafasi yake, muda wa kucheza na namna anavyoenda na mfumo huenda yakauweka mustakabali wake katika mazingira magumu ya kushindwa kupenya mbele ya nyota waliopo ikizingatiwa kwamba wengi ni wazoefu kikosini.
Ingawa kushindwa kumsajili Kuminga siyo lazima iwe janga kwa Lakers, kwani ni miongoni mwa nyota NBA wanaoacha swali la “ângeweza kufanya nini?” na hakuna uhakika kubadilisha timu kutamgeuza ghafla kuwa nyota ambaye alionekana kuwa na uwezo wa kutisha. Hata hivyo, uamuzi wake umeiacha Lakers ikiwa na tatizo ambalo halijapatiwa suluhisho.