Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa mziki huu wa Slot, mjipange

SLOT Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Anfield imekuwa bize kwelikweli kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi ikijaribu kufanya usajili wa kuboresha kikosi chao kwa ajili ya kuwa na nguvu ya kutetea taji hilo msimu ujao.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imenyakua taji la Ligi Kuu England msimu wa 2024/25, lakini wala haitaki kubweteka.

Miamba hiyo ya Anfield imekuwa bize kwelikweli kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi ikijaribu kufanya usajili wa kuboresha kikosi chao kwa ajili ya kuwa na nguvu ya kutetea taji hilo msimu ujao.

Kocha Arne Slot alimaliza msimu wake wa kwanza Liverpool kwa kuongeza mchezaji mmoja tu kwenye kikosi chake, Federico Chiesa.

Lakini, sasa Mdachi huyo amefungua pochi kuhakikisha anatengeneza kikosi kitakachokuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao.

Kiungo mshambuliaji Florian Wirtz na beki wa pembeni Jeremie Frimpong wameshatua kwenye kikosi cha Anfield katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi wakitokea Bayer Leverkusen, wakati Milos Kerkez akitarajia kufanya vipimo vya afya ndani ya wiki huu baada ya ada ya Pauni 40 milioni kukubaliwa na Bournemouth.

Beki mpya na straika mpya bado wanaendelea kuwa kwenye mpango wa kikosi cha Liverpool katika dirisha hili na ndiyo maana wanapambana kunasa saini ya beki wa kati wa Marc Guehi na straika wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike.

Katika upande mwingine, Trent Alexander-Arnold na Caoimhin Kelleher wameachana na timu hiyo wakitimkia Real Madrid na Brentford mtawalia.

Jarell Quansah naye yupo kwenye mipango ya kujiunga na Leverkusen, huku kukiwa na orodha ya mastaa kadhaa wakidaiwa kuwa na mpango wa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Anfield.

Mchezaji anayehusishwa zaidi na mpango wa kuondoka ni straika Darwin Nunez. Staa huyo wa kimataifa wa Uruguay amekuwa na wakati mgumu akishindwa kupenya kwenye kikosi cha Slot na sasa kinachoripotiwa anaweza kuibukia Napoli.

Wakati zikibaki wiki zisizozidi nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya, ni wazi kabisa kikosi cha kwanza cha Slot kitakuwa na utofauti kabisa kwa msimu ujao tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

-Golini na ukuta; Alisson anatazamiwa kuendelea kukaa golini, lakini atakabiliwa na vita kali ya namba na kipa mpya kwenye kikosi,  Giorgi Mamardashvili. Liverpool ilimalizana na Valencia tangu mwaka jana kuhusu kipa huyo wa Georgia na atatua mwezi ujao kushindania namba kwenye goli la miamba hiyo ya Anfield. Mbele ya Alisson, kutakuwa na Virgil van Dijk na Ibrahima Konate, licha ya kwamba inamsaka pia Guehi.

Nahodha huyo wa Crystal Palace anataka kuhakikishiwa kuanza kikosi cha kwanza atakapotua Anfield. Kwenye nafasi ya mabeki wa pembeni, kutakuwa na vita ya Milos Kerkez na Jeremie Frimpong, huku Andy Robertson akiwa na kasheshe zito la kuhakikisha anapambana kuendelea kubaki na namba yake.

-Kiungo na ushambuliaji; Slot amekuwa na imani kubwa kwa Ryan Gravenberch baada ya kumbadili uchezaji wake kwa msimu uliopita, akinogesha safu ya kiungo na kuna mastaa wengine kama Alexis Mac Allister na Domink Szoboszlai.

Lakini, sasa Wirtz anaingia kwenye eneo hilo, ambalo litamfanya Szoboszlai kupambana kupata namba kwenye kikosi cha Slot.

Kwenye safu ya ushambuliaji, Mohamed Salah baada ya kuongeza mkataka, ataendelea kuwa nguzo kubwa kwenye eneo hilo.

Luis Diaz kama atabaki atanogesha zaidi, huku Cody Gakpo naye ataongeza nguvu katika eneo hilo kama ilivyo kwa wakali Diogo Jota, huku wakiwa sokoni kusaka saini ya straika Ekitike.