Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kompyuta yatabiri bingwa EPL 2025/26

KOMPYUTA Pict

Muktasari:

  • Ingawa kuna habari njema kiasi kwa Manchester United, kompyuta hiyo pia inatabiri Arsenal itavunja rekodi kwa msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: KOMPYUTA ya kisasa  imetabiri msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England kwa msimu wa 2025/26 baada ya ratiba zote kutangazwa juzi.

Ingawa kuna habari njema kiasi kwa Manchester United, kompyuta hiyo pia inatabiri Arsenal itavunja rekodi kwa msimu ujao.

Arsenal na Man United zitakutana katika wiki ya kwanza ya msimu ujao na mchezo utapigwa katika dimba la Old Trefford.

Baada ya kumaliza msimu uliopita kwenye nafasi ya 15 ambayo ni nafasi yao mbaya zaidi kuwahi kutokea, Manchester United wametabiriwa kupanda hadi nafasi ya tisa, ambayo ni mafanikio makubwa ukilinganisha na msimu uliopita.

Ingawa haitokuwa kwenye mbio za ubingwa, kompyuta ya BETSiE inatabiri itamaliza ikiwa pointi mbili tu nyuma ya nafasi za kufuzu kucheza kimataifa tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita na ilimaliza kwa tofauti ya alama 23 kutoka nafasi ya kufuzu michuano ya kimataifa.

Kwa upande wa Arsenal, bado inatarajiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini haitatwaa taji tena, kwa mujibu wa kompyuta hiyo, kwani inatarajiwa kumaliza nafasi ya pili kwa msimu mwingine.

Kama hilo litatokea, basi Arsenal itakuwa timu ya kwanza katika historia ya EPL  kumaliza nafasi ya pili mara nne mfululizo.

Mwezi Mei, Arsenal ilikuwa tayari imelingana na rekodi ya kumaliza nafasi ya pili mara tatu mfululizo, rekodi  ambayo iliiweka  pia  kati ya 1999 na 2001.

Kwa upande mwingine wa msimamo, Liverpool imetabiriwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu England lakini kwa tofauti ya pointi moja tu.

Baada ya kumaliza msimu uliopita na pointi 84 kiwango cha chini zaidi cha ubingwa tangu Leicester iliposhinda taji kwa pointi 81 mwaka 2016, kikosi cha Arne Slot kinatarajiwa kuambulia pointi 77 msimu ujao.

Hii itawaweka pointi mbili juu ya Arsenal, huku Manchester City ikimaliza nafasi ya tatu kwa pointi 74.

Chelsea inatarajiwa kumaliza nafasi ya nne kwa pointi 69, ikiwa na pengo la pointi nane dhidi ya Newcastle (nafasi ya tano) na pointi 11 dhidi ya Aston Villa (nafasi ya sita), hali inayoakisi msimamo wa timu sita bora wa msimu uliopita.

Tottenham, iliyomaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya 17, inatarajiwa kupanda nafasi 10 hadi nafasi ya saba na kufuzu Ligi ya Europa Conference.

Bournemouth na Crystal Palace znatarajiwa kumaliza zikiwa chini kidogo ya Manchester United (nafasi ya tisa).

Katika nusu ya chini ya msimamo, Brighton itamaliza juu ya Nottingham Forest, ambayo imetabiriwa kutopata  matokeo makubwa kama msimu uliopita, kisha watafuatiwa na Brentford, Fulham na Everton.

West Ham itamaliza nafasi ya 16, ikiwa ni nafasi mbili chini ya msimu uliopita.

Wolves itakuwa timu ya mwisho kusalia ligi kuu, ikimaliza pointi tisa  juu ya  Leeds United.

Kwa upande wa timu zitakazoshuka daraja, Burnley itashuka daraja ikiwa nafasi ya 19.

Sunderland inatabiriwa kushuka daraja moja kwa moja, ikiwa na pointi 29  ambazo ni kiwango cha juu kuliko timu zote zilizoshuka daraja msimu uliopita.