Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kompay adondoka, Bayen yatoa neno

KOMPANY Pict

Muktasari:

  • Pamoja na kukosekana katika mkutano wa waandishi wa habari, Kompany alikuwepo uwanjani kuiongoza Bayern Munich katika mechi hiyo dhidi ya Arsenal ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

MUNICH, UJERUMANI: MENEJA wa Bayern Munich, Vincent Kompany, Juzi Ijumaa Oktoba 23, 2026 alianguka ghafla mazoezini na kuwahishwa hospitali kupatiwa matibabu.

Nahodha huyo wa zamani wa Ubelgiji amekuwa hajisikii vizuri tangu mwanzoni mwa wiki hii kutokana na mashambulizi ya virusi.

Hali hiyo ilimfanya akose mkutano wa waandishi wa habari kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal, juzi Jumatano.

Pamoja na kukosekana katika mkutano wa waandishi wa habari, Kompany alikuwepo uwanjani kuiongoza Bayern Munich katika mechi hiyo dhidi ya Arsenal ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

KOMPA 01

“Kompany atafanyiwa vipimo hospitalini na ataendelea kuwa chini ya uangalizi mkubwa kwa siku kadhaa.

“Timu yake ya makocha ambayo anaiamini, itaendelea kukaimu majukumu. Kila mmoja ndani ya Bayern anamuombea uponyaji wa haraka,” imesema taarifa ya Bayern Munich.

Kompany ameiongoza Bayern Munich kutwaa mataji mawili mfululizo ya Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ kwa misimu miwili mfululizo tangu alipojiunga nayo mwaka 2024 akitokea Burnley.

Klabu za Manchester City na Burnley alizowahi kuzitumikia kwa nyakati tofauti, zote zimemuombea uponyaji wa haraka.

KOMPA 02

“Kila mmoja katika klabu ya Manchester City anamtakia nafuu ya haraka nahodha wetu wa zamani na gwiji wa klabu, Vincent Kompany. Pona haraka, Vinny.” ilisema taarifa ya City.

Baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Arsenal siku ya Jumatano, Kompany alisema:

“Kama kocha, daima unatamani kufanya kila kitu na kufanikisha kila jambo. Nilipata maambukizi makali ya virusi wiki iliyopita, na kwa kweli sikuzingatia hali ya mwili wangu. Hatimaye, mwili wangu ulifika mahali ukaniambia, ‘Acha sasa!’”

KOMPA 03

Kompany alikuwa amekosa baadhi ya mazoezi na mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal, lakini alikuwepo pembeni mwa uwanja usiku wa mchezo huo ingawa hakuwa mchangamfu.

Pia alitazama mchezo uliotangulia wa Bayern Munich, ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya RB Leipzig, akiwa ameketi kwenye benchi. Hata hivyo, hakufanya mahojiano na waandishi wa habari baada ya mchezo huo.

Kompany ana watoto watatu na mke wake, Carla, ambaye alikutana naye walipokuwa Manchester.

Maambukizi ya virusi aliyopata Kompany yalikuwa miongoni mwa mada zilizozungumziwa sana katika maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal siku ya Jumatano na ikielezwa kuwa angeweza kuukosa mchezo huo.

Awali kulikuwa na hofu kuwa kocha huyo ana matatizo ya moyo lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka kuonyesha kuwa huo ndiyo ugonjwa uliomfanya akadondoka.