Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kadi nyekundu ya Olise, Arsenal kicheko UEFACL

Muktasari:

  • Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anatarajiwa kuiongoza timu yake kusafiri kwenda Munich wiki ijayo kukabiliana na miamba hiyo ya Ujerumani, ambayo itamkosa Olise, mmoja wa wachezaji hatari katika safu yake ya ushambuliaji.

LONDON, England: ARSENAL imepata ahueni kuelekea mchezo wake dhidi ya Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya nyota wa timu hiyo, Michael Olise, kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Jumanne usiku.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anatarajiwa kuiongoza timu yake kusafiri kwenda Munich wiki ijayo kukabiliana na miamba hiyo ya Ujerumani, ambayo itamkosa Olise, mmoja wa wachezaji hatari katika safu yake ya ushambuliaji.

Olise alitolewa nje katika kipindi cha pili dhidi ya Viking ya Norway, baada ya kujikuta katika mabishano na mshambuliaji wa timu hiyo, Zlatko Tripic.

Bayern ilikuwa imepindua matokeo kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuongoza 3-2 kupitia Harry Kane na Luis Diaz, lakini mambo yalibadilika dakika ya 74 baada ya Olise kuonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya mpinzani wake.

Wakati mwamuzi akimuonyesha kadi hiyo, winga huyo wa zamani wa Crystal Palace alikasirika na kuutupa mpira usoni mwa Tripic, kitendo kilichomfanya mwamuzi kuamua kumwonyesha kadi nyekundu.

Iwapo uamuzi huo hautafutwa kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal, kocha wa Bayern, Vincent Kompany, atalazimika kukikabili kikosi cha Arteta bila huduma ya mmoja wa nyota wake muhimu.

Mbali na pigo hilo, Bayern pia italazimika kujitathmini baada ya kushindwa kupata ushindi dhidi ya Viking, timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1992/93.

Viking ilipata bao la kusawazisha dakika ya 90 kupitia Herman Haugen na kuondoka na pointi moja dhidi ya Bayern, ambayo ni miongoni mwa timu zinazotajwa kuwania taji hilo.

Bao la Viking lililofungwa dakika ya pili lilikuwa miongoni mwa mabao ya mapema zaidi kufungwa dhidi ya Bayern katika kipindi cha hivi karibuni, baada ya Robin Fellhauer wa Augsburg kufunga ndani ya sekunde nane katika mchezo wa Bundesliga Jumamosi iliyopita.

Bayern sasa italazimika kurekebisha udhaifu wake wa kuanza michezo kwa kuyumba ikiwa inataka kufanya vizuri dhidi ya Arsenal wiki ijayo.

Arsenal, kwa upande wake, iliendeleza mwanzo mzuri katika hatua ya ligi baada ya kuichapa Lille mabao 3-0, ukiwa ni ushindi wa pili katika michezo yake miwili ya mwanzo.