KOMBE LAO: Makocha hawa wamefunika

Muktasari:
- Kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo ni mafanikio makubwa kwa kocha yeyote kwani inaonyesha uwezo alionao wa kuongoza timu na kushindana na zilizo bora zaidi ulimwenguni.
NEW YORK, MAREKANI: MASHINDANO la Klabu Bingwa ya Dunia ni moja ya michuano ya hadhi ya juu katika soka la klabu yanayowaleta pamoja mabingwa kutoka mabara mbalimbali duniani.
Kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo ni mafanikio makubwa kwa kocha yeyote kwani inaonyesha uwezo alionao wa kuongoza timu na kushindana na zilizo bora zaidi ulimwenguni.
Katika historia ya Kombe la Dunia la Klabu Bingwa kumekuwa na makocha walioweza kufika mara nyingi hatua hiyo muhimu ya fainali. Makala hii inachambua makocha waliotawala kwa kufika fainali nyingi zaidi

4. Zinedine Zidane - Fainali mbili
Tofauti na makocha wengine, Zidane akiwa na Real Madrid iliyokamilika alishinda taji hili mara mbili mfululizo mwaka 2016 na 2017, jambo ambalo halijawahi kufanywa na kocha yeyote katika historia ya michuano hiyo ambayo kwa msimu huu inayfanyikia Marekani.
Zidane aliongoza Real Madrid katika enzi ya mafanikio ya kipekee, akishinda fainali hizo mbili. Ufanisi huu ulimweka katika historia kama mmoja wa makocha wachache waliofanikiwa kushinda mashindano haya kwa asilimia 100 ya fainali alizofikia.

3. Rafael Benitez -Fainali TATU
Ni miongoni mwa makocha waliopoteza fainali nyingi za michuano hii. Alishinda taji kwa mara ya kwanza mwaka 2010 akiwa na Inter Milan, lakini alipoteza mara mbili akiwa na Liverpool 2005 kisha akapoteza tena 2012 akiwa na Chelsea.
Benítez ni kocha mwingine baada ya Pep Guardiola kufika fainali tatu akiwa na timu tatu tofauti.

2. Carlo Ancelotti - Fainali nne
Ancelotti amefika idadi sawa za fainali na Guardiola, lakini alipoteza moja kati ya nne alizowahi kutinga.
Kwa mara ya kwanza alifika fainali ya michuano hiyo mwaka 2007 akiwa na AC Milan ambapo timu hiyo ilishinda 4-2 dhidi ya Boca Juniors.
Baada ya hapo akaenda kushinda akiwa na Real Madrid mwaka 2014 dhidi ya San Lorenzo na akarudia tena mwaka 2022 mbele ya Al-Hilal.

1. Pep Guardiola-Fainali nne
Hadi sasa ndiye kocha pekee aliyecheza fainali nyingi za michuano hii bila ya kupoteza, pia ndio anayeongoza kwa kuvaa medali nyingi zaidi ya kocha yeyote.
Vilevile ndiye anaongoza kwa kutwaa taji akiwa na timu tatu tofauti.
Alianza kushinda taji la michuano hii akiwa na Barcelona mwaka 2009 kisha akafanya hivyo tena 2011 na timu hiyo hiyo.
Vilevile alishinda akiwa na Bayern Munich mwaka 2013 na Manchester City mwaka 2023.
MAKOCHA WENGINE
Mbali ya hao, makocha wengine wakubwa waliowahi kufika fainali za michuano hii ni pamoja na;
Luis Enrique – Barcelona (2015) – Taji 1
Sir Alex Ferguson – Manchester United (2008) – Taji 1
Jurgen Klopp – Liverpool (2019) – Taji 1
Thomas Tuchel – Chelsea (2021) – Taji 1
Hansi Flick – Bayern Munich (2020) – Taji 1
Santiago Solari – Real Madrid (2018) – Taji 1