Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia U-20  kuna mechi nne za kibabe

KOREA Pict

Muktasari:

  • Mechi ya kwanza ya Kundi C itawakutanisha Ghana na Korea Kusini mechi itakayopigwa Uwanja wa Arena Soswoinec kesho saa 10 jioni, mechi nyingine itakuwa kati ya Ufaransa na Ecuador saa 1 usiku.

KOMBE la Dunia la vijana U-20 raundi ya pili itaendelea tena kesho Septemba 9 nchini Poland huku mechi nne zikitarajiwa kuonyesha ushindani utakaowapa matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya 16 bora.

Mechi ya kwanza ya Kundi C itawakutanisha Ghana na Korea Kusini mechi itakayopigwa Uwanja wa Arena Soswoinec kesho saa 10 jioni, mechi nyingine itakuwa kati ya Ufaransa na Ecuador saa 1 usiku.

Kundi D itawakutanisha Italia dhidi ya New Zealand saa 12 jioni na nyingine ni kati ya Japan dhidi ya Marekani mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa Stadion Miejski.

Ghana ilianza kampeni yake kwa kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Ecuador, matokeo yaliyowaweka katika hali mbaya. Korea Kusini nayo haikuanza kwa ushindi baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Ufaransa. Hivyo, ushindi katika mchezo huu unaweza kuwa na thamani kubwa kabla ya mechi ya mwisho ya makundi.

KORE 01

Kwa Ghana, changamoto kubwa itakuwa namna ya kuzuia makosa yaliyowapa Ecuador nafasi ya kutawala mchezo uliopita. Kikosi hicho pia kinahitaji kupata jibu katika safu ya ushambuliaji baada ya kushindwa kufunga katika mchezo wa kwanza.

Korea Kusini, kwa upande mwingine, itaingia ikiwa na imani kutokana na namna ilivyoweza kuizuia Ufaransa na kupata sare. Timu hiyo inahitaji kutumia uzoefu wake katika mashindano haya ili kuongeza presha kwa Ghana.

Italia itaingia  ikiwa na nafasi ya kutengeneza historia baada ya kuanza kwa ushindani katika kundi linalozikutanisha timu zenye uzoefu mkubwa. Kundi D lina Japan, Marekani, New Zealand na Italia na ni miongoni mwa makundi magumu kutokana na historia ya timu hizo katika ngazi hii.

KORE 02

Japan na Marekani ni mechi yenye uzito mkubwa zaidi, kwani timu hizo zinakutana katika kundi hilo likiwa ni pambano la timu mbili zenye historia kubwa kwenye Kombe la Dunia la Wanawake U-20.

Japan ni miongoni mwa timu zilizobeba taji mwaka 2018, wakati Marekani ni moja ya mataifa yenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano haya ikiwa na mataji matatu.

Marekani pia imeingia Poland ikiwa na kikosi chenye uzoefu mkubwa wa kimataifa. Baadhi ya wachezaji wake walishiriki Kombe la Dunia U-17, huku wengine wakiwa tayari wamecheza kwenye mashindano ya U-20.