Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi hizi zitavunjwa Kombe la Dunia 2026

REKODI Pict

Muktasari:

  • Lakini mbali na mbio za ubingwa, Kombe la Dunia litashuhudiwa rekodi ambazo zimewahi kuishi kwa zaidi ya miongo miwili tangu mashindano hayo yaanzishwe mwaka 2002 nchini Canada, lakini hazijavunjwa.

TOLEO la 12 la mashindano ya Kombe la Dunia la vijana U-20 linaendelea kupigwa Poland huku mataifa 24 yakisaka taji ambalo limewahi kuzalisha mastaa kama Marta, Alex Morgan, Sydney Leroux na Asisat Oshoala.


Lakini mbali na mbio za ubingwa, Kombe la Dunia litashuhudiwa rekodi ambazo zimewahi kuishi kwa zaidi ya miongo miwili tangu mashindano hayo yaanzishwe mwaka 2002 nchini Canada, lakini hazijavunjwa.

Sasa je mwaka huu rekodi hizo zinaweza kuvunjwa au zitaendelea kuishi. Mwanaspoti imekuchambulia rekodi saba ambazo zimewekwa kwenye mashindano hayo.


REKO 01

USHINDI WA AJABU

Mwaka 2024 nchini Colombia timu ya taifa ya Ufaransa iliitandika Fiji mabao 11-0 katika hatua ya makundi na kuweka rekodi ya kupata ushindi mnono zaidi kwenye historia ya mashindano hayo.


Matokeo hayo yalivunja rekodi ya ushindi wa mabao tisa iliyokuwa ikishikiliwa na Korea Kaskazini dhidi ya Argentina mwaka 2012, Brazil dhidi ya Papua New Guinea mwaka 2016, pamoja na ushindi mwingine wa Brazil na Canada dhidi ya Fiji mwaka 2024.

Mashindano ya mwaka huu yameiongezwa kutoka timu 16 hadi 24

tofauti ya viwango kati ya baadhi ya mataifa inaweza kufanya rekodi hiyo iwe hatarini.


REKO 02

MABAO MENGI ZAIDI

Katika soka la wanawake vijana, mabao ni jambo la kawaida. Hata hivyo, hakuna mchezo uliowahi kuzidi mabao 11 yaliyofungwa kwenye ushindi wa Ufaransa dhidi ya Fiji mwaka 2024.

Kabla ya hapo, imewahi kushuhudiwa mabao 10 baada ya Ujerumani kuichapa Mexico 9-1 mwaka 2006, huku Ujerumani na China wakitoa sare ya kusisimua ya mabao 5-5 mwaka 2014.


REKO 03

REKODI YA WAFUNGAJI

Hadi sasa Mmarekani Sydney Leroux ndiye anaongoza kwenye listi ya wafungaji bora wa muda wote akiweka kambani mabao 10 sawa na Alexandra Popp wa Ujerumani akifanya hivyo mwaka 2010 wakati Christine Sinclair wa Canada aliweka rekodi hiyo tangu mwaka 2002.

Nyuma yao wapo Marta wa Brazil, Anja Mittag wa Ujerumani na Kelly Wilson wa Marekani, wote wakiwa na mabao tisa.

Kile kinachofanya rekodi ya Leroux kuwa ya kipekee ni kwamba aliianza kufunga akiwa na umri mdogo kabla ya kuja kuwa nyota wa timu ya taifa ya Marekani.

Leroux alianza kuonyesha uwezo wake akiwa na miaka 14 tu, aliposhiriki Kombe la Dunia la U-19 mwaka 2004 akiwa na timu ya Canada, kabla ya kubadili uraia na kuichezea Marekani.


REKO 04

HATTRICK

Christine Sinclair anashikilia rekodi ya kufunga mabao matano akifanya hivyo mwaka 2002 kwenye ushindi wa Canada wa mabao 6-2 dhidi ya England, mshambuliaji huyo alifunga mabao matano peke yake, rekodi ambayo baadaye ilikuja kufikiwa na Kim Un-Hwa wa Korea Kaskazini alipofunga mabao matano dhidi ya Argentina mwaka 2012.

Wengine waliofunga mabao manne kwenye mchezo mmoja ni Asisat Oshoala wa Nigeria, Stina Blackstenius na Liana Joseph wa Ufaransa.


REKO 05

SEKUNDE 14 TU!

Rekodi nyingine ni bao la haraka, mwaka 2014 nchini Canada, Courtney Dike wa Nigeria alihitaji sekunde 14 pekee kuifungia Super Falconets dhidi ya Korea Kusini mpaka leo hakuna mchezaji aliyewahi kuivunja.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba nafasi ya pili pia inashikiliwa na Mnigeria, Asisat Oshoala aliyefunga baada ya sekunde 31 dhidi ya New Zealand katika mashindano hayo hayo.

Hii inaonyesha jinsi kizazi cha Nigeria cha mwaka 2014 kilivyokuwa na kasi na ukali wa kushambulia tangu filimbi ya mwamuzi inapulizwa.


REKO 06

UMRI MDOGO ZAIDI

Kabla hajawa mshambuliaji maarufu wa Marekani, Sydney Leroux aliingia kwenye historia akiwa na miaka 14 na siku 187 alipocheza Kombe la Dunia mwaka 2004.

Rekodi hiyo bado haivunjwa kwa zaidi ya miaka 20, mchezaji aliyekuwa anakaribia kuifikia ni Charlyn Corral wa Mexico aliweka historia mwaka 2006 alipofunga akiwa na miaka 14 na siku 341 dhidi ya Uswisi.

Leo Corral ni mmoja wa nyota wakubwa kuwahi kutokea Mexico, jambo linalodhihirisha namna mashindano haya yanavyotengeneza vipaji mapema.


REKO 07

KOCHA KIJANA

Siyo wachezaji pekee walioweka rekodi.John Herdman aliiongoza New Zealand mwaka 2006 akiwa na miaka 31 na siku 29, na kuwa kocha mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya mashindano.

Baadaye Herdman alikuja kuwa mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi duniani baada ya kuinoa Canada na timu ya taifa ya wanaume ya Canada.


REKODI ZIKO HATARINI?

Mashindano ya mwaka huu yanaonekana kuwa na ushindani mkubwa kuliko yaliyopita. Marekani, Japan, Hispania, Korea Kaskazini, Nigeria na Brazil zote zina vikosi vyenye uwezo wa kushambulia kwa kasi.

Japan inafukuzia ubingwa wake wa pili tangu 2018, Nigeria inataka kuondoa rekodi ya kuwa washindi wa pili mara mbili, huku Hispania ikisaka kuendeleza ubabe wake katika soka la wanawake.

Lakini pamoja na vita ya kutwaa taji, macho yatakuwa kwenye vitabu vya historia. Je, kuna timu itakayovunja ushindi wa mabao 11? Je, kuna mshambuliaji atakayemzidi Leroux na Sinclair? Au sekunde 14 za Courtney Dike zitaendelea kubaki rekodi?