Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Misri ‘azimia’ baada ya wakeze kuzichapa baa, amtaliki mmoja

MISRI Pict

Muktasari:

  • Hossam alikuwa akifurahia mapumziko katika maeneo ya kifahari ya pwani ya Kaskazini mwa Misri, lakini hali ilibadilika na kuwa vurugu ndani ya mgahawa wa hoteli ya kifahari huko Porto Marina.

CAIRO, MISRI: KOCHA wa timu ya taifa ya Misri, Hossam Hassan, anadaiwa kuanguka baada ya wake zake wawili kupigana huku wakivutana nywele mbele ya watalii, kwa mujibu wa ripoti zilizosambaa.

Hossam alikuwa akifurahia mapumziko katika maeneo ya kifahari ya pwani ya Kaskazini mwa Misri, lakini hali ilibadilika na kuwa vurugu ndani ya mgahawa wa hoteli ya kifahari huko Porto Marina.

Mzozo kati ya mke wake wa muda mrefu, Howaida Al-Gharbawi, na mke wake wa pili, Dina “Dan Adam” Mustafa, ulianza ndani ya baa ya hoteli kabla ya kugeuka kuzichapa mbele ya watu. Ndugu waliingilia kati haraka, huku ulinzi wa hoteli wakiitwa kudhibiti hali hiyo.

Wanawake hao wawili walidaiwa kupata majeraha, ikiwemo mikwaruzo na michubuko.

Msongo wa mawazo uliotokana na tukio hilo la hadharani ulimuelemea Hossam ambaye kwa mujibu wa Al Arabiya, alizimia alipokuwa akijaribu kuamua ugomvi huo.

MISR 01

Hata hivyo, kwa mujibu wa Sky News Arabia, wakili wake alikanusha taarifa alizoziita kuwa ni uvumi kwamba Hassan alikuwa amepata tatizo la kiafya, akisema kocha huyo alikuwa katika hali nzuri.

Baada ya tukio hilo, kocha huyo wa Misri anadaiwa kumtaliki mke wake wa kwanza, Howaida, ambapo inadaiwa kwamba alisaini nyaraka za talaka katika ofisi ya msajili wa kisheria jijini Cairo.

Hossam alikuwa ameishi na Howaida kwa miongo kadhaa kabla ya kutengana kwao ghafla, na wawili hao wana watoto watatu.

Mohamed Shams, wakili wa mke wa pili, Dan Adam, aliiambia Sky News Arabia: “Tulitumaini kwamba suala hili lisingefikia hatua ya talaka, lakini mambo yalifikia kiwango hiki.”

MISR 02

Shams pia alisema mteja wake alipata “shambulio lililopangwa” wakati wa mapumziko yao huko Porto Marina.

Kwa upande mwingine, Ahmed Hamad, wakili wa familia ya Howaida, alikataa kuzungumzia kwa undani suala la kutengana kwao, akisema familia hiyo imeamua kutotoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa sasa.

Hossam alifunga ndoa na Dan Adam mwaka 2015, wakati akiwa kwenye ndoa na Howaida. Wawili hao walitengana kwa muda mwaka 2022 kabla ya baadaye kurudiana.

Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, mwanaume anaruhusiwa kisheria kuoa hadi wake wanne

Hossam amekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri tangu mwaka 2024, na aliiongoza hadi hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026, ambako ilitolewa baada ya kufungwa mabao 3-2 na Argentina katika mchezo uliopigwa jijini Atlanta. Baadaye, kocha huyo aliongeza mkataba na timu ya taifa hadi mwaka 2030.