Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klabu za England zashindana matumizi

EPL Pict
EPL Pict

Muktasari:

  • Na huko Manchester United hali ni tofauti kabisa. Klabu sasa zimebakiza muda usiozidi wiki nne za kusajili kabla ya dirisha halijafungwa na msimu kuanza.

LONDON, ENGLAND: LIVERPOOL pengine imetumia mkwanja mrefu kwenye usajili wa majira ya kiangazi, ikitumia zaidi ya Pauni 250 milioni, lakini Arsenal ndiyo timu iliyotumia pesa ndefu rasmi hadi sasa kwenye dirisha hili.

Na huko Manchester United hali ni tofauti kabisa. Klabu sasa zimebakiza muda usiozidi wiki nne za kusajili kabla ya dirisha halijafungwa na msimu kuanza.

Dirisha la usajili kwenye Ligi Kuu England litafungwa saa 1 usiku, Jumatatu ya Septemba 1. Lakini, Liverpool yenyewe imeshafanya dili zake mapema kabisa, ikitumia Pauni 252.2 milioni kunasa mastaa wapya, huku Pauni 116 milioni zikitumika kunasa huduma ya mchezaji mmoja, Florian Wirtz.

Wakali wengine walionaswa huko Anfield ni Hugo Ekitike, Milos Kerkez na Jeremie Frimpong, huku wachezaji Luis Diaz, Jarell Quansah, Caoimhin Kelleher, Trent Alexander-Arnold na Nat Phillips wakifunguliwa mlango wa kutokea jambo linaloifanya Liverpool kutumia pesa taslimu 137.7 milioni, kwa maana ya pesa zilizotumika kusajili toa zilizopatikana kwenye mauzo.

Lakini, Arsenal ndiyo timu iliyotumia pesa nyingi taslimu. Mastaa Martin Zubimendi, Noni Madueke na Viktor Gyokeres wote walijiunga na miamba hiyo ya Emirates kwenye dirisha hili, wakitumia Pauni 192.6 milioni.

Hata hivyo, yenyewe imeingiza Pauni 6.9 milioni tu kwenye mauzo ya Nuno Tavares na Marquinhos, hivyo kuifanya iwe imetumia pesa taslimu, Pauni 185.7 milioni kwa mujibu wa Transfermarkt.

Sera ya usajili kwenye kikosi cha Chelsea ziliendelea, ambapo imetumia zaidi ya Pauni 240 milioni kunasa mastaa wapya wanane, akiwamo Joao Pedro, Jamie Gittens, Jorrel Hato na Liam Delap. Manchester City imetumia Pauni 153.4 milioni, Man United (Pauni 131.5milioni) na Tottenham (Pauni 127.9milioni), kwenye orodha hiyo ya klabu zilizofanya matumizi makubwa hadi sasa.

Kiwango cha Man United kinaweza kuongezeka kama itafanikiwa kunasa huduma ya straika mpya, ambaye kwa sasa inamsaka Benjamin Sesko.

Lakini, Man United imepiga Pauni 20 milioni kutokana na wachezaji Anthony Elanga, Alvaro Carreras na Maxi Oyedele kuuzwa na timu zao na hivyo klabu hiyo ya Old Trafford ikipata gawio la bonasi ya kuwauza wakali hao.

Crystal Palace na Fulham ni klabu nyingine mbili ambazo zimepokea pesa za usajili kwenye dirisha hili, zikitumia Pauni 2 milioni na Pauni 400,000 mtawalia.

Aston Villa imetumia Pauni 6 milioni na kupokea Pauni 6 milioni na kufanya vitabu vyao vya hesabu kuwa sawa. Sunderland imetumia Pauni 121.6 milioni huku yenyewe ikiwa imeingiza Pauni 36.5 milioni kwenye mauzo ya Jobe Bellingham. Kuna klabu sita zimepata faida kwenye dirisha hili, ambazo ni Brighton, Wolves, Nottingham Forest, West Ham, Brentford na Bournemouth.