Kiungo Real Betis afungiwa kwa kumpiga Lamine Yamal
Picha na Mtandao
Muktasari:
- Katika mchezo huo, Bernal alitolewa nje baada ya kumshika Yamal shingoni kabla ya kumpiga kichwa mara mbili katika tukio lililozua mvutano uwanjani
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) imemfungia kiungo wa Real Betis, Facundo Bernal mechi nne baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshambulia mshambuliaji wa Barcelona, Lamine Yamal, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania ‘LaLiga’ uliofanyika Oktoba 17, 2026.
Katika mchezo huo, Bernal alitolewa nje baada ya kumshika Yamal shingoni kisha kumpiga kichwa mara mbili katika tukio lililozua mvutano uwanjani.
Picha na Mtandao
Tukio hilo lilitokea baada ya Real Betis kusawazisha na kufanya matokeo kuwa mabao 2-2, kabla ya Barcelona kuongeza kasi na kuibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Yamal naye alionyeshwa kadi ya njano wakati wa tukio hilo, huku mwamuzi akichukua hatua dhidi ya Bernal kwa kitendo chake cha kumshambulia mshambuliaji huyo wa Barcelona.
Picha na Mtandao
Adhabu hiyo inamaanisha Bernal atakosa michezo minne ijayo ya LaLiga ambayo ni dhidi ya Celta Vigo, Malaga na Elche pamoja na pambano la watani wa jadi dhidi ya Sevilla linalotarajiwa kuchezwa Novemba 22, 2026.
Kukosekana kwa kiungo huyo ni pigo kwa Real Betis, ambayo italazimika kucheza michezo hiyo bila huduma yake wakati ikiendelea na harakati za kusaka pointi katika ligi hiyo.