Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona yakimbilia UEFA kuishtaki PSG kisa bango

Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Barcelona imelalamikia bango hilo, ambalo lilionekana la kuwadhihaki mashabiki wa klabu hiyo, likiwa na ujumbe uliosomeka “Mauaji kwa Mtindo wa Paris”.

Paris, Ufaransa. Klabu ya Barcelona imewasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) dhidi ya PSG, ikipinga bango kubwa lililoonyeshwa na mashabiki wa klabu hiyo kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu hizo jana Jumanne Oktoba 20, 2026.

Bango hilo lilionyeshwa katika Uwanja wa Parc des Princes, likiwa na picha ya mtu aliyefunika uso kwa barakoa na kufanana na mhusika wa filamu za kutisha Michael Myers, akionekana kukata nembo ya Barcelona kwa msumeno wa umeme uliokuwa na damu.

Mashabiki wa PSG pia walitumia fataki na vifaa vya kutoa mwanga majukwaani, hali iliyofanya ionekane kana kwamba cheche zilikuwa zikitoka kwenye msumeno huo wakati ukiharibu nembo ya Barcelona.

Barcelona iliona onyesho hilo kuwa la uchokozi uliopitiliza na lenye maudhui ya kuudhi, hivyo kuwasilisha malalamiko kwa UEFA kuhusu tukio hilo.

Gazeti la L'Equipe la Ufaransa liliripoti kuwa bango hilo kubwa lilikuwa limepata idhini ya PSG kabla ya kuonyeshwa uwanjani, jambo linalodaiwa kuongeza hasira za viongozi wa Barcelona.

Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa PSG iliwahi kukataa bango lililopendekezwa kwa mchezo wa Ligi ya Ufaransa dhidi ya Le Mans, ambalo lilihusishwa na machafuko ya kijamii nchini humo, lakini ikaruhusu bango lililoilenga Barcelona.

Inadaiwa kuwa klabu hiyo ilitangaza onyesho hilo kupitia mfumo wa matangazo wa uwanja kabla ya bango kufunuliwa.

Wakati huo huo, wajumbe wa Barcelona waliomba mabango mengine yaliyokuwa na lugha chafu dhidi ya klabu yao yaondolewe wakati wa mchezo.

Malalamiko hayo yanaibua mjadala kuhusu mipaka ya ubunifu wa mashabiki katika kuandaa mabango makubwa yanayojulikana kama tifo, hasa pale yanapokuwa na picha za vurugu au ujumbe unaoweza kutafsiriwa kuwa wa kuudhi.

Hata hivyo, haijathibitishwa iwapo UEFA imefungua rasmi uchunguzi au imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya PSG kufuatia malalamiko hayo.

PSG na Barcelona zimekuwa zikivuta hisia za mashabiki kila zinapokutana katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku ushindani wao ukivutia hisia za mashabiki ndani na nje ya uwanja.

Katika mchezo huo, PSG iliibuka na ushindi wa mabao 4-2.