Kiungo Ecuador autaja ubora wake
Muktasari:
- Flores alifunga bao moja dakika ya nne akipiga shuti la umbali wa zaidi ya yadi 40 lililomshinda kipa katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ghana kwenye mchezo wao wa kwanza wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-20.
KIUNGO wa Ecuador, Rosa Flores ametaja sababu ya kuonyesha kiwango bora kwenye mechi dhidi ya Ghana akisema hilo limesababishwa na kujituma na kushirikiana na wenzake.
Flores alifunga bao moja dakika ya nne akipiga shuti la umbali wa zaidi ya yadi 40 lililomshinda kipa katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ghana kwenye mchezo wao wa kwanza wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-20.
Flores amesema bao hilo lilikuwa moja ya bao lake bora kwani alilifanyia kazi mazoezini na kufunga kwenye mechi hiyo ya kwanza ya kundi C.
“Nguvu yangu kubwa ni kupiga mashuti kutoka nje ya boksi. Nina furaha sana na nimefurahishwa na kufunga kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi yangu ya kwanza,” amesema Flores
Kiungo huyo anayekipiga LDU Quito hakufunga tu bao, bali alitoa asisti ya bao la pili lilofungwa na Domenica Arboleda dakika ya 17 kabla Arboleda mwenyewe hajakamilisha ushindi wa Ecuador kwa bao la tatu mwishoni mwa mchezo.
“Nafikiri ushindi huo ni muhimu sana kwetu na umetupa morali kubwa ya kuangalia tunakwendaje kwenye mechi ya pili ambayo ni muhimu tupate tena pointi tatu ili kujiweka sehemu salama. Ushindi huo umeiweka Ecuador katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenda hatua ya 16 bora, kabla ya kukutana na Ufaransa na Korea Kusini katika michezo miwili inayofuata.