Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Liverpool, Alexander Isak astopishwa

ISAK Pict

Muktasari:

  • Dirisha hili Newcastle imekataa ofa kutoka Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden na kusisitiza hatouzwa kwa ada ya chini ya Pauni 120 milioni.

NEWCASTLE, ENGLAND: KOCHA wa Newcastle United, Eddie Howe amefunguka alilazimika kumpa ruhusa straika wao Alexander Isak kutokuwepo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Celtic kutokana na presha kubwa ambayo mchezaji huyo anakumbana nayo kwa sasa kuhusu tetesi za kwenda Liverpool.

Dirisha hili Newcastle imekataa ofa kutoka Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden na kusisitiza hatouzwa kwa ada ya chini ya Pauni 120 milioni.

Isak mwenye umri wa miaka 25 alisafiri kwenda Glasgow kutoka kambini, Austria Ijumaa ya wiki iliyopita kwa ajili ya mchezo dhidi ya Celtic uliomalizika kwa Newcastle kushinda mabao 4-0, lakini hakuonekana uwanjani.

Kutokuwepo kwake kuliibua maswali zaidi kuhusu hatma yake, lakini kocha Howe alisisitiza mchezaji huyo kwa asilimia 100 atakuwa safarini pamoja na timu Alhamisi ya wiki hii kwenda Singapore kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu na aliongeza aliamua mwenyewe kumweka Isak nje ya mchezo huo kutokana na presha kubwa iliyokuwepo kuhusu tetesi namashabiki walikuwa wakihitaji kumwona, hivyo aliona kusingekuwa na utulivu na asingeweza kucheza mechi katika kiwango kinachohitajika.

“Isak alikuwa nasi muda wote huko Austria, lakini kutokana na tetesi na mambo yanayoendelea, niliamua kumrudisha nyumbani. Jambo la mwisho aliloniomba lilikuwa ni kukaa jukwaani bila kucheza lakini niliona haitokuwa heshima kwake. Kwa kuwa tulikubaliana hatocheza leo, tulionani bora asiwepo kabisa,” alisema Howe na kuongeza hana uhakika wa asilimia 100 ikiwa mshambuliaji huyo atakuwa naye msimu ujao.

“Ni vigumu kutoa uhakika wa asilimia 100 kwa mchezaji yeyote. Hilo si jambo ninaloweza kufanya kwenye soka, maana lolote linaweza kutokea. Ninachoweza kusema ni Isak ana furaha sana kuwa hapa. Anawapenda wachezaji wenzake, benchi la ufundi na klabu kwa jumla. Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, wawakilishi wa Isak walikuwa tayari kujadili ofa ya Liverpool kwa sababu wanahitaji mchezaji wao aongezwe mshahara kutoka Pauni 130,000 kwa wiki anaoupokea kwa sasa.

Hata hivyo, dili hilo linaonekana kuwa gumu kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika na Newcastle.