Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa jota uwanja wafungiwa Saudi Arabia

JOTA Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Jota, alifariki dunia Julai mwaka jana akiwa na umri wa miaka 28 baada ya kupata ajali ya gari. Alikuwa rafiki wa karibu wa Neves, ambaye aliwahi kucheza naye katika klabu ya Wolverhampton Wanderers na timu ya taifa ya Ureno.

SAUDI ARABIA: Klabu ya Al-Taawoun inayoshiriki Ligi Kuu Saudi Arabia, imeamriwa kucheza michezo miwili ya ligi nyumbani bila mashabiki baada ya wafuasi wake kumkejeli kiungo wa Al-Hilal, Ruben Neves, kuhusu kifo cha rafiki na aliyekuwa mwenzake katika timu ya taifa ya Ureno, Diogo Jota.

Mbali na adhabu hiyo, Al-Taawoun imepigwa faini ya Riyal 100,000 za Saudi Arabia, sawa na takriban pauni 20,000 (Sh68 milioni).

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Jota, alifariki dunia Julai mwaka jana akiwa na umri wa miaka 28 baada ya kupata ajali ya gari. Alikuwa rafiki wa karibu wa Neves, ambaye aliwahi kucheza naye katika klabu ya Wolverhampton Wanderers na timu ya taifa ya Ureno.

JOT 01

Kwa heshima ya Jota, Neves sasa anavaa jezi namba 21 katika timu ya taifa ya Ureno, huku akiwa na mchoro wa tattoo kwenye ndama ya mguu wake unaowaonyesha yeye na Jota wakikumbatiana. Pia alikuwa miongoni mwa waliobeba jeneza wakati wa mazishi ya Jota.

Kabla ya mchezo wa Jumamosi uliomalizika kwa Al-Hilal kushinda mabao 6-0, mashabiki wa Al-Taawoun walimlenga Neves kwa kurudia kwa sauti jina “Jota” mara kadhaa.

Baada ya mchezo huo, Neves aliwaambia waandishi wa habari:

JOT 02

“Natumaini tu hawataenda kusali baadaye baada ya walichokifanya.”

Cristiano Ronaldo, anayekipiga katika klabu ya Al-Nassr nchini Saudi Arabia na aliyekuwa mwenzake Jota katika timu ya taifa, alitoa wito mashabiki waliohusika kufungiwa kuhudhuria michezo kwa maisha yao yote.

JOT 03

Katika taarifa yake, Al-Taawoun ilisema: “Tabia ya aina hii haikubaliki kabisa na haiwakilishi klabu, mashabiki wake wala maadili ambayo klabu inajulikana nayo.

“Ushindani wa michezo hauwezi kuwa sababu ya kuwatukana, kuwadharau au kuwanyanyasa wengine kwa gharama ya hisia za mtu yeyote.”