Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo awavaa mashabiki

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo lilitokea wakati Al Hilal ikiifunga Al Taawoun 6-0, ambapo baadhi ya mashabiki wa  Al Taawoun walidaiwa kutumia jina la Diogo Jota katika nyimbo zilizomlenga Neves.

RIYADH, SAUDI ARABIA: CRISTIANO Ronaldo ametaka mashabiki waliohusika na vitendo vya kumdhalilisha Ruben Neves, wakati wa mchezo kati ya Al Taawoun na Al Hilal wapigwe marufuku kuhudhuria mechi maisha yao yote.

Tukio hilo lilitokea wakati Al Hilal ikiifunga Al Taawoun 6-0, ambapo baadhi ya mashabiki wa  Al Taawoun walidaiwa kutumia jina la Diogo Jota katika nyimbo zilizomlenga Neves.

Jota, ambaye alikuwa rafiki wa karibu na Neves, alifariki katika ajali ya gari mwaka 2025.

Neves alionekana kuathirika na tukio hilo, huku Ronaldo akilaani vikali tabia hiyo na kusema hakuna nafasi ya vitendo kama hivyo katika soka.

Baada ya tukio hilo, Al Hilal iliwasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Soka Saudi Arabia, huku Al Taawoun ikisema iko tayari kushirikiana na mamlaka katika uchunguzi.

Shirikisho la Soka Saudi Arabia pamoja na uongozi wa Ligi Kuu pia wamekemea tukio hilo, wakisema kutumia msiba wa mtu kama njia ya kuwachokoza wengine hakukubaliki.

Uchunguzi umeanzishwa na hatua zinatarajiwa kuchukuliwa dhidi ya waliohusika.

Ronaldo, ambaye ni nahodha wa Al Nassr, ameonyesha msimamo mkali. akitaka adhabu kali ili kuzuia matukio kama hayo kujirudia katika viwanja vya Saudi Arabia.