Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Guardiola, Rodri ataka kutimkia Real Madrid

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Rodri ni mmoja kati ya mastaa ambao wamepata mafanikio makubwa akiwa na Man City tangu alipojiunga nayo msimu wa 2018-2019 akikaa kwenye kikosi hicho kwa misimu saba, amecheza michezo 298 na kufunga mabao 28 akiwa ametwaa makombe manne ya Ligi Kuu England na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

REAL Madrid ina imani kubwa ya kumsajili kiungo Rodri kutoka Manchester City baada ya tetesi za kuondoka kwa Kocha Pep Guardiola mwisho wa msimu huu. Kiungo huyo wa Hispania, 29, anaonekana kuwa miongoni mwa malengo makubwa ya Madrid dirisha hili la usajili.

Taarifa zinasema baada ya Guardiola kuonekana kuwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo, mawakala wa Rodri walifanya mazungumzo haraka na Real Madrid ili kupambania dili hilo, staa huyo aweze kujiunga nao mwishoni mwa msimu huu.

Rodri ni mmoja kati ya mastaa ambao wamepata mafanikio makubwa akiwa na Man City tangu alipojiunga nayo msimu wa 2018-2019 akikaa kwenye kikosi hicho kwa misimu saba, amecheza michezo 298 na kufunga mabao 28 akiwa ametwaa makombe manne ya Ligi Kuu England na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, anaweza kukutana na wakati mgumu kutokana na aina ya wachezaji ambao kocha anayekwenda kwenye timu hiyo Jose Mourinho anawahitaji kwenye kikosi chake.


John Stones

BAYERN Munich wanapanga kufanya usajili wa kushtukiza kwa beki wa timu ya Taifa ya England na klabu ya Manchester City, John Stones.

Nyota huyo mwenye miaka 31 anatajwa kuwa tayari kuondoka Man City mwishoni mwa msimu zikiwa ni taarifa ambazo zimezuka siku chache baada ya Kocha Pep Guardiola kuelezwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Bayern ambao ni mabingwa wa Ujerumani wanataka kuimarisha safu ya beki.


Bernardo Silva

ATLETICO Madrid inafikiria kufanya usajili wa viungo wawili wakubwa, Bernardo Silva wa Manchester City na beki wa Chelsea, Marc Cucurella ili kuboresha kikosi chao msimu ujao kiwe na makali kwenye Ligi Kuu Hispania, La Liga pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha Diego Simeone ameshatangaza anawataka mastaa hao. Msimu huu unaofikia ukingoni wikiendi ijayo, Atletico imecheza mechi 37 na ina pointi 69 katika msimamo wa La Liga.


Casemiro

INTER Miami wako karibu kukamilisha usajili wa kiungo wa Brazil, Casemiro kutoka Manchester United.

Mchezaji huyo mwenye miaka 34 anatarajiwa kuondoka Old Trafford mwisho wa msimu, ingawa mashabiki wengi wa timu hiyo hawataki kiungo huyo aondoke kwenye timu hiyo kipindi hiki kutokana na kiwango cha juu ambacho alikionyesha msimu huu wa ligi akiiongoza timu hiyo kuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.


Alisson Becker

KIPA wa Liverpool na timu ya taifa ya Brazil, Alisson Becker anataka kujiunga na Juventus majira haya ya joto hata kama klabu hiyo haitafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Juventus imekuwa kwenye rada za kipa huyo kwa muda mrefu na sasa inaonekana kuwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Becker mwenye umri wa miaka 33, msimu huu amecheza jumla ya mechi 34 za michuano yote.


Marcus Rashford

Barcelona imekubaliana masuala binafsi na mshambuliaji wa England, Marcus Rashford kuhusu mkataba wa kudumu, lakini bado hawajafikia makubaliano ya ada ya usajili na Manchester United.

Hivi karibuni iliripotiwa mshambuliaji huyo anataka kubaki kwenye kikosi hicho ambacho amekipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania La Liga. Rashford yupo Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja wenye kipengele cha kumnunua jumla.


Bazoumana Toure

Liverpool wameonyesha rasmi nia ya kumsajili winga wa TSG Hoffenheim, Bazoumana Toure mwenye umri wa miaka 20. Hata hivyo, wanakabiliwa na ushindani kutoka Manchester United, Aston Villa na Newcastle United ambazo nazo zinamtaka.

Liverpool inataka kuboresha kikosi chao baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu huu wa Ligi Kuu England ambao unatarajiwa kumalizika Jumapili ijayo.


Jadon Sancho

Borussia Dortmund hawana mpango wa kumrudisha kwa mara ya tatu winga wa Manchester United, Jadon Sancho ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Aston Villa ambayo ametwaa nayo ubingwa wa Europa League.

Staa huyo amekuwa akiondoka na kurudi kwenye timu hiyo lakini kwa sasa timu hiyo inataka kumwachia jumla ili akatafute maisha sehemu nyingine na Villa pia inataka kumchukua jumla.