Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kifo cha Brandon Clarke chazua utata Marekani

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa mwandishi Michael Babcock wa TMZ Sports, mamlaka zinazochunguza tukio hilo zinaangalia uwezekano wa Clarke kufariki kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kupita kiasi.

MEMPHIS, MAREKANI: KIFO cha mchezaji wa zamani wa kikapu wa timu Memphis Grizzlies, Brandon Clarke kimeishtua dunia alipotangazwa juzi, Jumanne kufariki dunia, huku taarifa zaidi na uvumi ukiendelea kuibuka kuhusu mazingira yaliyosababisha kifo chake.

Kwa mujibu wa mwandishi Michael Babcock wa TMZ Sports, mamlaka zinazochunguza tukio hilo zinaangalia uwezekano wa Clarke kufariki kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kupita kiasi.

“Bado haijafahamika nini hasa kilitokea, lakini tukio hili linachunguzwa kama kuna uwezekano wa matumizi ya dawa nyingi zaidi. Mamlaka zilipata vitu vinavyohusishwa na matumizi ya dawa za kulevya eneo la tukio. Kutokana na hilo, wanaangalia kama kulikuwa na matumizi ya dawa nyingi zaidi kama sababu inayoweza kuwa imechangia kifo cha kijana huyu ambaye alikuwa na afya nzuri,” alisema Babcock.

Babcock aliongeza kuwa Clarke, ambaye alitangazwa kufariki dunia muda mfupi baada ya mamlaka kumkuta katika nyumba moja mjini Los Angeles. Awali, alionekana kuwa katika hali nzuri siku chache kabla ya kifo cha ghafla.

“Tulizungumza na kinyozi wake ambaye alikuwa naye Ijumaa usiku. Walikuwa wakitazama pamoja mechi za mchujo za NBA wakati akinyolewa. Hakukuwa na dalili yoyote kwamba kuna tatizo au jambo lisilo la kawaida,” alisema.

Clarke, ambaye katika misimu ya hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, alicheza michezo miwili pekee msimu huu wa 2025-26. Katika misimu saba aliyocheza NBA, nyota huyo wa zamani wa Gonzaga alikuwa na wastani wa pointi 10.2 na ribaundi 5.5 kwa kila mchezo. Clarke alikuwa na umri wa miaka 29.

Grizzlies watoa salamu za rambirambi

Timu ya Memphis Grizzlies, iliyomaliza msimu wa mwisho wa Clarke katika nafasi mbaya baada ya kushinda michezo 25 na kupoteza 57, ilitoa taarifa rasmi kuelezea masikitiko yake juu ya kifo hicho.

Clarke alizaliwa Septemba 19, 1996 huko Canada na alianza kucheza kikapu akiwa chuoni kabla ya kuchaguliwa kama chaguo (draft) la 21 na Oklahoma City Thunder 2019 kabla ya kuuzwa kwenda Memphis Grizzlies. Aliitwa katika kikosi cha NBA All-Rookie First Team na pia alishiriki mashindano ya Rising Stars Challenge 2020.