Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiboko ya Yamal, halafu haringi

YAMAL Pict

Muktasari:

  • Mchezaji mwenyewe ni beki wa kushoto wa Paris Saint-Germain, Nuno Mendes - ambaye anashangaza wengi kuona jina lake wala halimo kwenye orodha ya wanaopigiwa upatu kunyakua Ballon d’Or.

PARIS, UFARANSA: ANAJUA boli, halafu wala haringi. Mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na supastaa wa mataji matatu makubwa kwa msimu uliopita, ametamba alimzima mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa kwenye soka kwa sasa, akimtaja Lamine Yamal.

Mchezaji mwenyewe ni beki wa kushoto wa Paris Saint-Germain, Nuno Mendes - ambaye anashangaza wengi kuona jina lake wala halimo kwenye orodha ya wanaopigiwa upatu kunyakua Ballon d’Or.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 22 aliwasha moto kwenye fainali ya Nations League na kuisaidia Ureno kuichapa Hispania, Jumapili iliyopita na alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi.

Alifunga bao maridadi kabisa la kusawazisha kwa shuti la chini kufanya ubao usomeke 1-1. Kisha alifunga pia mkwaju wake wa penalti katika kipindi cha kupigiana mikwaju hiyo, Ureno iliposhinda 5-3.

Katika mechi hiyo, alihusika kwenye bao la pili lililofungwa na Cristiano Ronaldo, ambalo lilikuwa la kusawazisha kuwa 2-2, huku akimpa somo la kutosha winga wa Barcelona na Hispania, Yamal, ambaye amekuwa akipigiwa debe na kupewa nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’Or ya mwaka huu.

Mendes alisema: “Ilikuwa vita na Yamal kama vita nyingine tu nilizopambana na wachezaji wengine msimu huu. Nimekutana na wachezaji wengi sana mahiri, mafundi ambao walikuwa na uwezo wa kufanya jambo kubwa, lakini hii ya sasa nilimzima Lamine na kumnyima fursa ya kufanya kile ambacho amekuwa bora.

"Hii ilisaidia timu na nimefurahi nimesaidia timu yangu kushinda hili taji. Nimecheza mechi nyingi na ni suala la kujituma binafsi pamoja na kufanya vyema na makocha wangu PSG na Ureno.

“Ballon d'Or? Nacheza na Ousmane (Dembele) na amekuwa na msimu bora, Lamine naye amekuwa na msimu bora. Lakini, Ousmane atakuwepo kwenye Kombe la Dunia la Klabu na Lamine hatakuwapo, hivyo namfurahia Ousmane. Namtakia kila la heri kwenye Ballon d'Or, mimi na wachezaji wengine tutamsaidia.

“Mimi nacheza soka langu, kuna wachezaji wanaokaribia hiyo tuzo, sijaweka akili yangu huko.”

Kwenye mchakamchaka wa tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu, mastaa wanaopewa nafasi kubwa ya kuibuka washindi ni staa wa Barcelona, Yamal, mkali wa PSG, Dembele na supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah.

Katika mechi hiyo ya fainali, Nuno Mendes aligusa mpira mara 80, pasi 47, amefunga bao moja, amelala yombo mara tatu, amekokota mpira kwa mafanikio mara nne na ameshinda vita za ana kwa ana mara saba.

WANAOBETI WATAJA 10 WENYE UWEZO  WA KUBEBA BALLON  D'OR MWAKA HUU

1.Ousmane Dembele

2.Lamine Yamal

3.Nuno Mendes

4.Mohamed Salah

5.Raphinha

6.Kylian Mbappe

7.Khvicha Kvaratskhelia

8.Desire Doue

9.Gianluigi Donnarumma

10.Lautaro Martinez