Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya Man City bado hukumu tu!

Muktasari:

  • Man City imeshtakiwa na Ligi Kuu England kufanya makosa 115 yanayohusu kukiuka kanuni za matumizi Financial Fair Play, katika mashtaka yaliyofunguliwa Februari mwaka huu.

MANCHESTER,  ENGLAND: KUMEKUCHA. Suala la kusikiliza pande zote mbili kwenye kesi ya mashtaka ya Ligi Kuu England dhidi ya Manchester City limekamilika, imeripotiwa.

Man City imeshtakiwa na Ligi Kuu England kufanya makosa 115 yanayohusu kukiuka kanuni za matumizi Financial Fair Play, katika mashtaka yaliyofunguliwa Februari mwaka huu.

Miamba hiyo ya Etihad, Man City imekana kutenda makosa hayo na kudai itapambana kwa nguvu zote kujitetea katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa kwenye kituo cha International Dispute Resolution Centre cha huko London, tangu katikati ya mwezi Septemba.

Lakini, kwa mujibu wa ripoti, hatua ya kusikiliza kesi hiyo imeshakamilika.

Hilo ni kwa mujibu wa The Daily Mail, ambayo imedai pande zote mbili zimetoa maelezo yao ya ushahidi kwenye kamati husika.

Sasa kamati ya watu watatu itakwenda kujifungia kuchakata ushawishi huo kabla ya kuutolea hukumu ambayo itawekwa wazi duniani kote.

Hata hivyo, hukumu ya kesi hiyo haiwezi kutangazwa hivi karibuni kutokana na wingi wa ushahidi uliotolewa ambao utahitaji mchakato wa muda kiasi.

Kinachoelezwa ni itachukua miezi kadhaa kabla ya miamba hiyo ya Ligi Kuu England, Man City kutambua hatima yao. Ishu ya Man City kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni za udhibiti wa matumizi imefanyika kwa zaidi ya miaka 14.

Mwanzoni Man City ilifunguliwa mashtaka 115, ambayo yaliongezeka na kufikia 130 kutokana na ishu za utawala.

Man City imeshutumiwa kushindwa kutoa ripoti sahihi ya hesabu zao za kifedha na matumizi kwa kipindi cha miaka tisa kati ya msimu wa 2009-10 na 2017-18. Ilishutumiwa pia kushindwa kutoa taarifa za kutosha za kuhusu malipo ya kocha wao wa zamani, Roberto Mancini, alivyokuwa akilipwa kati ya msimu wa 2009-10 na 2012-13.

Mashtaka hayo yanahusisha pia kushindwa kuwasilisha mishahara ya wachezaji wao waliyolipa kati ya msimu wa 2010-11 na 2015-16. Katika hilo hilo la kufanya makosa kwenye masuala ya kifedha, Man City nayo ilishutumiwa kushindwa kutoa usharikiano wakati wa uchunguzi uliofanywa na Ligi Kuu England.

Uchunguzi ulianza baada ya kuibuka na taarifa Man City ilifanya udanganyifu wa matumizi ya fedha iliyochapishwa kwenye gazeti la Germanmagazine Der Spiegel mwaka 2018. Kama itakutwa na hatia, inaweza kukumbana na adhabu ya kupigwa faini na kupokwa pointi.

Inaweza pia kushushwa daraja endapo kama itagundulika kufanya makosa makubwa zaidi.

Klabu hiyo itakata rufaa endapo kama hukumu itatolewa dhidi yao, jambo ambalo linatoa tafsiri kwamba uamuzi wa mwisho kabisa unaweza kusifikiwe juu ya kesi hiyo hadi mwisho wa msimu ujao. Man City imekuwa ikikanusha kufanya makosa hayo tangu yalipochapishwa kwa mara ya kwanza na kwamba inaamini ushahidi wake utaifanya kesi hiyo kumalizika na kuisafisha timu yao kwenye madai hayo mazito.

Kikosi hicho cha Man City kinachonolewa na Pep Guardiola kitashuka uwanjani leo Jumatano kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus utakaofanyika Turin, Italia.