Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kane asaini Bayern Munich hadi 2029

KANE Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anaendelea kung'ara akiwa katika kiwango bora cha maisha yake ya soka, akifunga mabao 50 katika mwaka huu wa kalenda na kuonekana miongoni mwa vinara wa kuwania tuzo ya Ballon d'Or.

LONDON, ENGLAND: NAHODHA wa England, Harry Kane, amekubali kuongeza mkataba mpya wa miaka mitatu utakaomuweka Bayern Munich hadi mwaka 2029, hatua inayozima matumaini ya vigogo wengine wa Ulaya waliokuwa wakifuatilia huduma yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anaendelea kung'ara akiwa katika kiwango bora cha maisha yake ya soka, akifunga mabao 50 katika mwaka huu wa kalenda na kuonekana miongoni mwa vinara wa kuwania tuzo ya Ballon d'Or.

Kane, ambaye ameiongoza England hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia, alikuwa akifuatiliwa na klabu kadhaa kubwa barani Ulaya, ikiwemo Barcelona, huku mustakabali wake ukisubiriwa kwa hamu.

KAN 01

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo amefikia makubaliano ya mdomo na mabingwa hao wa Ujerumani kuhusu mkataba mpya, huku Bayern ikitarajiwa kukamilisha taratibu za kiofisi kabla ya kuutangaza rasmi.

Mkataba huo mpya utamuweka Kane Allianz Arena hadi mwaka 2029, atakapokuwa na umri wa miaka 36.

Awali, Kane na Bayern walikuwa wakisisitiza kuwa hakukuwa na haraka ya kuamua hatma yake kabla ya majira ya kiangazi. Akizungumza mwezi Mei, mshambuliaji huyo amesema wakati huo haukuwa sahihi kujadili suala hilo, akisisitiza kuwa hakukuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi.

“Si wakati wa kuzungumzia hilo sasa, lakini hakuna hofu. Tulitaka kufanya mazungumzo mwishoni mwa msimu na bado tuna Kombe la Dunia la kucheza. Kila mtu anajua jinsi ninavyofurahia maisha yangu hapa. Hali iko shwari,” amesema Kane.

KAN 02

Mkataba wake wa awali ulikuwa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, baada ya kusaini mkataba wa miaka minne alipojiunga na Bayern akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2023 kwa ada ya pauni 100 milioni.

Kane anaripotiwa kulipwa takribani pauni 400,000 kwa wiki nchini Ujerumani, ingawa bado haijafahamika kama mkataba mpya utakuja na ongezeko la mshahara.

Mbali na mafanikio uwanjani, Kane na familia yake wamezoea maisha ya Ujerumani. Nahodha huyo na mke wake, Kate, pamoja na watoto wao wanne, wamekuwa wakishiriki shughuli mbalimbali za kijamii, zikiwemo sherehe za jadi za Oktoberfest.

Familia hiyo ilihamia Ujerumani kutoka Kaskazini mwa London miaka mitatu iliyopita, na makubaliano hayo mapya yanaashiria kuwa hawana mpango wa kurejea England hivi karibuni.


KAN 03

AENDELEA KUVUNJA REKODI

Kane amekuwa akivunja rekodi mbalimbali akiwa na klabu na timu ya taifa ya England.

Katika mapumziko ya hivi karibuni ya mechi za kimataifa, alifikisha mechi 125 akiwa na England na kuifikia rekodi ya Peter Shilton ya mechi nyingi zaidi kwa timu hiyo. Anatarajiwa kuongeza idadi hiyo katika mechi zijazo.

Kwa upande wa Bayern, Kane aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefikisha mabao 100 katika Bundesliga kwa kasi zaidi, akihitaji mechi 98 pekee kufikia idadi hiyo.

Pia aliweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika mechi 50 za kwanza za mchezaji katika Bundesliga, baada ya kutikisa nyavu mara 55.

Katika kipindi chake Bayern, Kane tayari ameshinda mataji mawili ya Bundesliga, Kombe la Ujerumani pamoja na mataji mawili ya German Super Cup.