Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam wasiwachukulie poa Wamisri wao

AZAM Pict

Muktasari:

  • Hii mechi inatupa presha sana hapa kijiweni na kama tungekuwa huko Misri tungewachana ukweli wachezaji wa Azam FC kuwa wasiichukulie poa.

LEO lambamba wa Azam FC wapo ugenini huko Misri wakikipiga na ZED FC ya huko kuanzia mida ya saa mbili usiku.

Hii mechi inatupa presha sana hapa kijiweni na kama tungekuwa huko Misri tungewachana ukweli wachezaji wa Azam FC kuwa wasiichukulie poa.

Maana sisi huku Tanzania tumekuwa na utamaduni wa kudharau au kuiogopa mechi kabla hatujacheza kwa kuangalia tu historia au eneo ambalo inatoka.

Sasa kwa mfano kwa kule Misri sisi tunaamini timu tishio kwenye mashindano ya kimataifa za nchi ile ni Al Ahly, Zamalek na Pyramids.

Kwamba hizo ukipangwa kukutana nazo basi una kigongo lakini nyingine zilizobakia za nchi hiyo tunaona tunazimudu kabla hatujacheza nazo na hapo ndo huwa tunajichanganya.

Tunapeana tahadhali mapema ili Azam FC isiingie kwa kuwachukulia poa hao Wamisri ambao wanakutana nao kwa vile sio wapinzani wepesi na wakifanya masihara wanaweza kuwatoa.

ZED huwa wanapiga mpira mkubwa sana kwenye mechi zao na ni timu ambayo imekuwa ikipenda kushambulia pasipo kuogopa aina ya mpinzani ambaye inakutana naye kwenye mechi husika.

Ligi ya Misri ni ngumu na ukiona timu inaweza kupata ushindi dhidi ya wababe kama Zamalek tena kwa kushinda mabao matatu halafu ikiwa uwanja wa ugenini hiyo sio timu ya kawaida.

Hivyo Azam iiendee mechi hiyo kama inacheza na wale wababe wengine wa pale Misri.