Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kama Infantino akiondoa? hawa kumrithi FIFA

Muktasari:

  • Infantino, ambaye analenga muhula wa nne na wa mwisho madarakani, anahitaji kura 106 kati ya wanachama 211 wa FIFA ili ashinde uchaguzi huo. Hata hivyo, hali imeanza kubadilika baada ya baadhi ya vyama vya soka, vikiwemo vya England na Wales, kuonyesha kutoridhishwa na uongozi wake.

LONDON, England: SHINIKIZO dhidi ya Rais wa FIFA, Gianni Infantino, linaendelea kuongezeka huku baadhi ya vyama vya soka duniani vikianza kuondoa barua zao za kumuunga mkono kuelekea uchaguzi mkuu wa Machi mwakani.

Infantino, ambaye analenga muhula wa nne na wa mwisho madarakani, anahitaji kura 106 kati ya wanachama 211 wa FIFA ili ashinde uchaguzi huo. Hata hivyo, hali imeanza kubadilika baada ya baadhi ya vyama vya soka, vikiwemo vya England na Wales, kuonyesha kutoridhishwa na uongozi wake.

Mbali na hilo, Baraza la FIFA linaweza kuitisha kikao cha dharura na kujadili uwezekano wa kumng'oa madarakani kabla hata ya uchaguzi.

Iwapo safari ya Infantino itafikia tamati, majina manne yanaonekana kujitokeza kwa nguvu kuwania nafasi hiyo.


VICTOR MONTAGLIANI, MWANAMAGEUZI KUTOKA CONCACAF

Rais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF), Victor Montagliani, anatajwa kuwa mmoja wa wagombea wenye nguvu.

Mtendaji huyo wa Canada alichaguliwa mwaka 2016 akiwa na ajenda ya kuimarisha utawala bora, kama alivyofanya Infantino mwanzoni mwa uongozi wake.

Montagliani alicheza nafasi kubwa katika maandalizi na uendeshaji wa Kombe la Dunia la 2026 lililoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico.

Akiwa na uzoefu mkubwa wa kisiasa ndani ya soka, amewahi kupinga wazi wazo la kuongeza Kombe la Dunia hadi timu 64 na pia hakukubaliana na mpango wa kucheza Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili.


SHEIKH SALMAN, NGUVU KUTOKA ASIA

Rais wa Shirikisho la Soka Asia (AFC), Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa, naye anaonekana kuwa mpinzani mkubwa wa Infantino.

Kiongozi huyo wa Bahrain ameiongoza AFC tangu mwaka 2013 na chini yake mashindano ya bara hilo yamepanuka kwa kiwango kikubwa, ikiwemo kuzinduliwa kwa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake, pamoja na kuongezwa kwa idadi ya timu kwenye Kombe la Mataifa ya Asia.

Sheikh Salman pia amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa namna FIFA inavyoendeshwa chini ya Infantino na anaungwa mkono na mataifa mengi ya Asia.


NASSER AL-KHELAIFI, HANA HAMU

Rais wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi, pia ametajwa kama mmoja wa watu wenye uwezo wa kuongoza FIFA kutokana na ushawishi wake mkubwa ndani ya soka la Ulaya.

Baada ya kusambaratika kwa mradi wa European Super League mwaka 2021, Al-Khelaifi aliongoza mabadiliko makubwa ndani ya chama cha klabu za Ulaya (ECA), akiongeza wanachama hadi zaidi ya klabu 800.

Hata hivyo, watu wake wa karibu wameweka wazi kuwa mfanyabiashara huyo wa Qatar hana mpango wa kugombea urais wa FIFA, licha ya kutajwa mara kwa mara.


MATTIAS GRAFSTROM, MTU WA NDANI WA FIFA

Katibu Mkuu wa FIFA, Mattias Grafstrom, ndiye jina jingine linalotajwa.

Grafstrom amekuwa mmoja wa watu wa karibu zaidi wa Infantino tangu mwaka 2016, kabla ya kuteuliwa rasmi kuwa Katibu Mkuu wa FIFA mwaka 2024.

Ingawa anaifahamu vizuri mifumo ya uendeshaji wa FIFA, ukaribu wake na Infantino unaweza kupunguza nafasi zake. Aidha, kuna mtazamo unaoibuka kwamba rais ajaye wa FIFA anapaswa kutoka nje ya bara la Ulaya.


MBIO ZA URAIS WA FIFA ZAHAMIA MOROCCO

Rais mpya wa FIFA anatarajiwa kuchaguliwa katika Mkutano Mkuu wa 77 wa FIFA, utakaofanyika Morocco mwezi Machi mwaka ujao. Wagombea wote wanapaswa kuwasilisha majina yao kabla ya Novemba 18.

Kwa sasa, macho ya dunia ya soka yanaelekezwa kwenye vita hiyo ya uongozi, huku hatma ya Infantino ikibaki kuwa moja ya mijadala mikubwa ndani ya FIFA.