Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yakodi ndege ya Sh1 trilioni

Muktasari:

  • Katika ziara hiyo, kikosi cha 'The Blues' kinatarajiwa kusafiri zaidi ya maili 25,000, kikianzia England, kupitia Australia na nchi mbalimbali za Asia kabla ya kurejea London, safari inayofanywa kwa kiwango cha juu cha anasa.

LONDON, England: CHELSEA imeweka wazi ukubwa wake nje ya uwanja baada ya kukodi ndege ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya Sh1 trilioni kwa ajili ya ziara yake ya maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Katika ziara hiyo, kikosi cha 'The Blues' kinatarajiwa kusafiri zaidi ya maili 25,000, kikianzia England, kupitia Australia na nchi mbalimbali za Asia kabla ya kurejea London, safari inayofanywa kwa kiwango cha juu cha anasa.

Kwa mujibu wa taarifa, Chelsea imekodisha Airbus A340-300 VVIP, moja ya ndege bora zaidi za binafsi duniani inayomilikiwa na kampuni ya AirX.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 100 kwa faraja ya hali ya juu, mizigo zaidi ya 1,000 na kuruka kwa hadi saa 16 bila kutua.

Makadirio yanaonyesha kuwa ndege mpya ya aina hiyo ina thamani ya karibu Pauni milioni 300 (zaidi ya Sh1 trilioni), ikiwa imewekewa huduma za kiwango cha juu ikiwemo sehemu ya mapumziko, viti vinavyogeuka kuwa vitanda, wahudumu wanane na huduma za chakula cha hadhi ya VIP.

Chelsea pia inadaiwa kutumia takribani Pauni 400,000 (zaidi ya Sh1.4 bilioni) kuikodisha ndege hiyo kwa safari moja pekee kutoka Australia hadi Hong Kong mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kikosi hicho kilisafiri pia kwa ndege hiyo kutoka Uwanja wa Ndege wa Gatwick nchini England hadi Sydney, Australia, ambako kilicheza mechi za kirafiki dhidi ya Western Sydney Wanderers na Tottenham.

Hata hivyo, bado haijathibitishwa kama Chelsea itaendelea kutumia ndege hiyo katika safari zake za kuelekea Indonesia, Malaysia na kurejea England.

Kwa mujibu wa kampuni ya AirX, Airbus A340-300 imeundwa mahsusi kwa ajili ya kusafirisha timu za michezo na makundi makubwa ya wasafiri wanaohitaji huduma za kiwango cha juu.

"Ndege hii ni chaguo bora kwa timu za michezo. Ina viti 100 vinavyogeuka kuwa vitanda, wahudumu wanane na huduma zinazobadilishwa kulingana na mahitaji ya abiria, kuanzia vitafunwa hadi chakula cha kifahari," ilieleza AirX.

Chelsea itaendelea na ziara yake kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Juventus mjini Kowloon, Hong Kong, kabla ya kukutana na AC Milan jijini Jakarta siku tatu baadaye. Baada ya hapo itacheza na Johor Darul Ta'zim nchini Malaysia, kisha kurejea Stamford Bridge kumalizia maandalizi dhidi ya Real Sociedad.