Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juventus yaongeza kasi dili la  Bernardo Silva

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Ripoti hizo zinaeleza Juventus imevutiwa sana na Silva kutokana na uzoefu na ubunifu wake ikiamini ataenda kuboresha aneo lao la kiungo.

JUVENTUS imepanga kuongeza juhudi zao dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kumsajili kiungo mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno, Bernardo Silva, ambaye anaripotiwa ataondoka mwisho wa msimu huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Italia Corriere dello Sport, Juventus inataka kuwapiku wapinzani wao wakubwa Ulaya, zikiwemo Atletico Madrid na Barcelona, ambao nao wameonyesha nia ya kuhitaji huduma ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31.

Ripoti hizo zinaeleza Juventus imevutiwa sana na Silva kutokana na uzoefu na ubunifu wake ikiamini ataenda kuboresha aneo lao la kiungo.

Hata hivyo,  mshahara wake unatajwa kuwa moja ya changamoto kubwa kwa klabu zinazomhitaji kwani fundi huyu anahitaji kulipwa kuanzia Pauni 300,000 kwa wiki.

Nyota huyu wa zamani wa AS Monaco, kuna uwezekano mkubwa pia akatimkia Saudi Arabia ambako timu kibao zipo tayari kumlipa takribani mara tatu ya mshahara wake wa sasa wa Pauni 300,000 kwa wiki anaoupata katika kikosi cha Man City.


Joao Pedro

MKURUGENZI wa michezo wa  Barcelona, Deco anaripotiwa alikuwepo katika Fainali ya Kombe la FA wikiendi iliyopita katika dimba la Wembley kumtazama mshambuliaji wa Chelsea, Joao Pedro, licha ya klabu yake kutokuwa tayari kumuuza.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail, Deco alikuwa uwanjani hapo ili  kufuatilia kwa karibu mwenendo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye amekuwa akionyesha uwezo mkubwa Chelsea.

Hata hivyo, mabosi wa Chelsea wanatajwa hawana mpango wa kumuuza kwa sasa, lakini Barca bado haijakata tamaa.


Georginio Wijnaldum

CONVERTY City wanaripotiwa kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo mkongwe wa Al-Ettifaq raia wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum, ambaye mkataba wake unamalizika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Coventry inafikiria kufanya mazungumzo ya awali ili kupata huduma ya kiungo huyo, 35, hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa katika Ligi Kuu England na mashindano ya Ulaya.

Wijnaldum, ambaye aliwahi kucheza kwa mafanikio makubwa Liverpool hata yeye inadaiwa kutamani kurudi England na kucheza soka la ushindani.


Loum Tchaouna

EVERTON inataka kumsajili winga chipukizi wa Burnley, Loum Tchaouna, mwenye umri wa miaka 22.

Kwa mujibu wa tovuti ya Football Insider, Everton inataka kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji wa pembeni na maskauti wao wamekuwa wakimfuatilia Tchaouna kwa muda mrefu na wameonekana kuvutiwa naye sana.

Hata hivyo, bado hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa Burnley kwa ajili ya fundi huyo anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya umri chini ya miaka 21.


Wilfried Gnonto

LEEDS United inaripotiwa ipo tayari kumruhusu mshambuliaji wao wa pembeni, Wilfried Gnonto kuondoka dirisha lijalo la majira ya kiangazi na SC Freiburg kutoka Ujerumani ni miongoni mwa klabu zinazohitaji saini yake.

Kwa mujibu wa Sky Sports Germany, Leeds ipo tayari kumuuza au kumtoa kwa mkopo wenye kipengele cha kumuuza mazima ikiwa ni sehemu ya mpango wao wa kutafuta pesa zitakazowawezesha kusajili dirisha lijalo.

Gnonto, 22, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Hata hivyo, mazungumzo baina ya timu hizo bado hayajaanza.


Alessandro Bastoni

BARCELONA imeendelea kumfuatilia kwa karibu beki kisiki wa Inter Milan, Alessandro Bastoni, lakini mchezaji huyo, 27, inadaiwa hadi sasa bado hajafanya uamuzi wowote.

Taarifa za ndani zinadai Barcelona inamtazama Bastoni kama mmoja wa mastaa wanaoweza kuboresha safu yao ya ulinzi ikiwa itaipata huduma yake.

Kwa sasa Inter Milan haina mpango wa kumruhusu ingawa inaweza kufanya hivyo ikiwa itawasilishwa ofa nono mezani. Ripoti zinaongeza, Bastoni hana presha ya kuondoka.


Douglas Luiz

JUVENTUS inadaiwa kuwa na mpango wa kumrudisha au kumpa nafasi nyingine kiungo wao wa kimataifa wa Brazil, Douglas Luiz, ikiwa itashindikana kumuuza dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport, Juventus bado haijafanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo, 28.

Luiz, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Aston Villa, inadaiwa kuwekwa sokoni na vigogo wa Juventus ambao wanahitaji pesa kwa ajili kufanyia usajili wa mastaa wengine.


Charles De Ketelaere

BAYERN Munich inaripotiwa kuwa na nia ya kumsajili winga wa Atalanta, Charles De Ketelaere, lakini kwa sasa kipaumbele chao ni mshambuliaji wa Newcastle United, Anthony Gordon na ikishindikana ndio itarudi kwa De Ketelaere.

De Ketelaere, 25, amekuwa na msimu mzuri akiwa na Atalanta na ameendelea kuonyesha maendeleo makubwa baada ya kipindi kigumu alichopitia awali akiwa AC Milan.

Hadi sasa bado hakuna mazungumzo rasmi yaliyoanza kati ya Bayern na Atalanta.