Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juventus yajipanga kumnyakua Federico Chiesa Liverpool

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Taarifa zinaeleza kwamba uongozi wa Juventus unaamini kurejea kwa Chiesa kunaweza kuongeza kasi na ubunifu katika safu ya ushambuliaji, hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye Ligi Kuu Italia (Serie A).

JUVENTUS inatafakari uwezekano wa kumrejesha Italia aliyekuwa staa wake, Federico Chiesa, 28, ambaye kwa sasa yupo Liverpool.

Taarifa zinaeleza kwamba uongozi wa Juventus unaamini kurejea kwa Chiesa kunaweza kuongeza kasi na ubunifu katika safu ya ushambuliaji, hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye Ligi Kuu Italia (Serie A).

Hata hivyo, bado haijulikani kama Liverpool itakuwa tayari kumruhusu nyota huyo kuondoka ingawa dalili zinaonyesha kwamba timu hyo itakubali kumwachia ili kupata pesa itakazotumia kufanyia usajili wa mastaa wengine inaowataka katika dirisha dogo la Januari.

Mkataba wa sasa wa Chiesa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2028, lakini tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote, akifunga mabao mawili na kutoa asisti tatu.

Chiesa amekuwa akihusishwa kuondoka Liverpool tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza.


Sandro Tonali

JUVENTUS ina nafasi ndogo ya kumsajili kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali, 25, katika dirisha la usajili la Januari.

Mabosi wa Newcastle hawataki kumuuza Tonali katika dirisha lijalo kwani ni sehemu muhimu ya mipango ya kocha Eddie Howe kwa msimu huu.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa vigogo hao wa Turin hawajakata tamaa na wanaamini wanaweza kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.


Maghnes Akliouche

TOTTENHAM Hotspur inafikiria kufanya jaribio la kumsajili kiungo mshambuliaji wa Monaco, Maghnes Akliouche, 23, katika dirisha lijalo la usajili.

Akliouche ambaye ni raia wa Ufaransa, anaweza kuuzwa na Monaco kwa takribani Pauni 40 milioni, lakini kiasi hicho kinaweza kuwa kikubwa zaidi ikiwa timu zinazomtaka zitaongezeka.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2028. Msimu huu kacheza mechi tatu, ana asisti tano.


Elliot Anderson

MABINGWA wa zamani wa England, Manchester City, wana imani kubwa ya kuwapiku Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, Elliot Anderson, 23.

Anderson ameonyesha kiwango bora msimu huu, hali iliyovutia klabu kadhaa kubwa Ulaya, lakini majirani hao wawili ndio wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumpata.


Christopher Nkunku

FENERBAHCE imewasilisha ofa ya mazungumzo kwa ajili ya kumsajili straika wa AC Milan na timu ya taifa ya Ufaransa, Christopher Nkunku, 28.

Taarifa zinaeleza timu hiyo inaamini Nkunku anaweza kuongeza ubora katika kikosina mchezaji mwenyewe anaonekana kuwa tayari kujiunga nayo.

Kwa sasa mabosi wa AC Milan wanafanya majadiliano ya ofa iliyowasilishwa inayodaiwa kufikia Pauni 30 milioni.


James McAtee

LEEDS United imepata pigo kubwa katika juhudi za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, James McAtee, 23, kuelekea dirisha lijalo.

Inaelezwa kwamba mchezaji huyo anataka kujiunga na timu ya nje ya England licha ya uwepo wa timu kibao zinazohitaji saini yake ndani ya nchi hiyo.

Hadi sasa Forest bado haijatoa msimamo wa mwisho kuhusu mustakabali wa staa huyo ikiwa itamuuza au la.


Oscar Bobb

MABINGWA wa zamani England, Manchester City, wako tayari kumtoa kwa mkopo winga wa kimataifa wa Norway, Oscar Bobb, 22, katika dirisha hili la usajili.

Miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kumsajili ni Borussia Dortmund ambayo inamtaka kwa mkopo wa nusu msimu.

Dortmund inakumbana na ushindani kutoka Crystal Palace, Bournemouth na Newcastle United.


Nico Schlotterbeck

REAL Madrid imejiunga rasmi katika vita ya kutaka kumsajili beki wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani, Nico Schlotterbeck, 26.

Taarifa kutoka Hispania zinaeleza Dortmund iko tayari kumwachia ikiwa kuna timu itawasilisha ofa ya takribani Pauni 60 milioni.

Real Madrid inatafuta beki wa kati kwa ajili ya kuboresha safu ya ulinzi ambayo mastaa wengi huenda wakaondoka misimu miwili ijayo.