Joan Garcia kuiwahi El Clasico
Muktasari:
- Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alisajiliwa kutoka Espanyol msimu huu ambapo alipata jeraha la goti wiki iliyopita ambalo lilihitaji upasuaji, akitarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda.
Kipa wa Barcelona, Joan Garcia, huenda akarudi uwanjani, Oktoba 26, 2025 wakati wa mechi ya La Liga dhidi ya Real Madrid, kulingana na ripoti za klabu hiyo ya Catalunya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alisajiliwa kutoka Espanyol msimu huu ambapo alipata jeraha la goti wiki iliyopita ambalo lilihitaji upasuaji, akitarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda.
Mwandishi wa AS, Javi Miguel, ameripoti kwamba Garcia anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mechi dhidi ya Real Madrid itakayofanyika Oktoba 26, 2025 baada ya kupewa muda wa kupona kati ya wiki 4 hadi 6, huku akitarajiwa kuzikosa mechi dhidi ya Paris Saint-Germain, Sevilla, Girona na Olympiacos mwezi ujao kutokana na jeraha lake la meniscus.
Wojciech Szczesny atachukua nafasi ya Garcia, huku Marc-André ter Stegen naye akiwa nje kwa miezi kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji msimu huu wa joto.
Septemba 28, 2025, Szczesny alicheza mechi yake ya kwanza msimu huu wakati Barcelona ikiichapa Real Sociedad mabao 2-1.