Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'ADIOS' Busquets aaga, kustaafu soka

ADIOS Pict

Muktasari:

  • Busquets alianza maisha yake ya soka akiwa na vigogo wa Catalonia, Barca na alikuwa mchezaji tegemeo kati ya mwaka 2008 na 2023 katika moja ya vikosi bora zaidi katika historia ya mpira wa miguu, akishirikiana na nyota kama Lionel Messi, Xavi na Andres Iniesta.

BARCELONA, HISPANIA: KIUNGO wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa anaichezea Inter Miami, Sergio Busquets ametangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu akiwa na umri wa miaka 37.

Busquets alianza maisha yake ya soka akiwa na vigogo wa Catalonia, Barca na alikuwa mchezaji tegemeo kati ya mwaka 2008 na 2023 katika moja ya vikosi bora zaidi katika historia ya mpira wa miguu, akishirikiana na nyota kama Lionel Messi, Xavi na Andres Iniesta.

Kiungo huyo fundi alishinda mataji tisa ya LaLiga, Ligi ya Mabingwa mara tatu na Kombe la Mfalme (Copa del Rey) mara saba akiwa na Barca, pamoja na Kombe la Dunia la 2010 akiwa na Hispania.

Katika video ya kuaga aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram jana, Busquets alisema: "Habari zenu nyote. Nahisi kuwa muda umefika wa kuachana na maisha ya soka kama mchezaji wa soka wa kulipwa.

ADI 01

Soka limenipa uzoefu wa kipekee kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu. Nina kumbukumbu nyingi za furaha tangu ikiwa mtoto mdogo, kutoka timu kama Badia hadi kikosi cha akiba cha Barca, nikapita pia Barbera, Lleida na Jabac, nisema asante sana kwa FC Barcelona, klabu ya maisha yangu.

Sehemu ambayo nilitimiza ndoto zangu na nikavaa jezi niliyopenda sana. Nilisherehekea mataji mengi na kuwa na wakati wa kipekee Camp Nou ambao siwezi  kuusahau."

"Asante pia kwa timu ya taifa ya Hispania. Ilikuwa heshima kuichezea na kupata mafanikio ambayo daima yatadumu. Asante Inter Miami kwa kuniruhusu kuwa sehemu ya klabu yenu. Asante kwa wachezaji wenzangu  wote, benchi la ufundi na kila mtu niliyewahi kushirikiana naye."

ADI 02

Asante kwa mashabiki wote duniani kwa mapenzi na heshima mliyonionyesha, nina matumaini nimeweza kuonyesha hata kwa udogo yale ambayo mlihitaji kuyaona kutoka kwangu."

Busquets alicheza mechi 722 akiwa na Barcelona kabla ya kuondoka mwaka 2023 kutokana na matatizo ya kifedha yaliyokuwa yanaikabili timu hiyo.

ADI 03

Baada ya hapo alitua Inter Miami na alicheza mechi 105, akishinda Supporters’ Shield na Leagues Cup akiwa chini ya timu hiyo inayomilikiwa na David Beckham.

Akiwa katika kikosi hicho cha Inter, Busquets amecheza sambamba na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona, Messi, Jordi Alba na Luis Suarez.