Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Deco amtabiria makubwa Gavi, amlinganisha na Puyol, Xavi 

DECO Pict

Muktasari:

  • Gavi, mwenye umri wa miaka 21, alikuzwa kupitia akademi maarufu ya La Masia, na alipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa mwaka 2021, ingawa amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Licha ya umri wake mdogo, kiungo huyo amekuwa na sifa ya kuonyesha juhudi zisizoisha na mwenye kipaji cha kiufundi.

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, anaamini nahodha wa kikosi hicho, Gavi atafikia hadhi ya kuwa gwiji wa klabu hiyo kama Xavi Hernandez na Carles Puyol, endapo atajitolea maisha yake yote ya soka klabuni hapo.

Gavi, mwenye umri wa miaka 21, alikuzwa kupitia akademi maarufu ya La Masia, na alipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa mwaka 2021, ingawa amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Licha ya umri wake mdogo, kiungo huyo amekuwa na sifa ya kuonyesha juhudi zisizoisha na mwenye kipaji cha kiufundi.

Kwa sasa Gavi atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitano baada ya kufanyiwa upasuaji kutibu jeraha la meniscus ya ndani kwenye goti lake la kulia, kama ilivyothibitishwa na Barcelona kwenye taarifa yao rasmi.

Katika mahojiano na Mundo Deportivo, Deco ameeleza kuvutiwa kwake na Gavi, akimsifu kama mchezaji aliyekamilika.

DE 01

“Nilisema msimu uliopita, Gavi ni mchezaji ambaye hawezi kubadilishwa, ana tabia ya kipekee, ni mchezaji kamili. Amekuwa katika kiwango hiki kwa muda mrefu na ana miaka 21 tu... Amekuwa katika timu ya kwanza kwa karibu miaka mitano. Msimu uliopita ulikuwa mgumu kwake kutokana na majeraha ya mara kwa mara, labda sikutarajia kuendelea kulizungumzia, lakini kwa upande mwingine, yeye ni mchezaji wa Barça wa maisha. Natumai atakuwa kama Xavi, kama Puyo, waliokua hapa na kuwa magwiji wa klabu,” amesema Deco.

Deco pia amesisitiza kuwa Barcelona inamchukulia kiungo huyo kijana kama sehemu ya msingi wa utambulisho wa klabu na mustakabali wake huku akibainisha kuwa, kumkosa katika kipindi cha takribani miezi mitano. 

DE 02

“Ni pigo kwa sasa, lakini jambo muhimu zaidi ni Gavi wa miaka ijayo. Uamuzi kuhusu upasuaji, kulingana na maelezo ya madaktari, ni kwa ajili ya kumhifadhi Gavi wa baadaye. Ni ngumu kwake na kwetu pia, lakini tunapaswa kufikiria zaidi ya msimu huu. Gavi ni rasilimali ya klabu, mchezaji ambaye atakuwa wa kihistoria kwa klabu. Tunamuhurumia sana kwa kumkosa miezi hii, lakini hili litakuwa muhimu kwa mustakabali wa kazi yake ya soka,” amefafanua huku akisema Barcelona haina mpango wa kusajili baada ya jeraha la Gavi.

Akizungumza zaidi, Deco amekanusha uvumi kwamba Barcelona watakimbilia sokoni kutokana na jeraha la muda mrefu la Gavi. Alisisitiza kuwa klabu haina mpango wa kuuza wachezaji wala kusajili kwa haraka bila mpango, kwani kikosi kilicho sasa kina uwezo wa kukabiliana na changamoto.

DE 03

“Wazo letu lilikuwa wazi kutouza mchezaji yeyote isipokuwa akiomba kuondoka. Kuwa Barça ni kitu cha kipekee; sidhani kama kuna kitu bora zaidi, lakini kila mchezaji ana ulimwengu wake, mazingira yake; kila mmoja ni tofauti. Sisi tunafikiria kitu kimoja, lakini huenda mchezaji anafikiria vingine.

“Kikosi hiki kina njaa ya ushindi, wanataka kushinda, wako vizuri, tuna chumba cha kubadilishia nguo chenye vipaji vya hali ya juu vya kibinadamu, na sidhani kama kuna yeyote anayetaka kuondoka kwani hatujapokea maombi yoyote. Kwa kuwa na wachezaji wengi, makocha wanapaswa kusimamia kwa sababu si kila mtu atacheza, lakini kuwa na ubora na watu waliopo kunakuwezesha kuziba mapengo ya ghafla. Katika sehemu hii ya mwanzo, tumepoteza baadhi ya wachezaji, lakini mwishowe, tunadumisha kiwango na kuendelea kushinda,” amesema.

DE 014

Barcelona kwa sasa inaongoza msimamo wa La Liga baada ya wapinzani wao wakuu, Real Madrid, kupoteza alama mwishoni mwa wiki. Mchezo wao unaofuata utakuwa dhidi ya Paris Saint-Germain katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kesho Jumatano, Oktoba 1, 2025.