Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jezi ya Pele yauzwa sh13 bilioni

JEZI Pict

Muktasari:

  • Jezi hiyo ni ambayo Pele aliivaa katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Sweden mwaka 1958 ambayo timu yake Brazil iliibuka na ushindi wa mabao 5-2.

NEW YORK, MAREKANI: JEZI ya gwiji wa zamani wa soka duniani, hayati Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’, imenunuliwa kwa kiasi cha Dola 4.9 milioni (Sh13 bilioni) katika mnada uliofanyika juzi Alhamisi, jijini New York, Marekani

Jezi hiyo ni ambayo Pele aliivaa katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Sweden mwaka 1958 ambayo timu yake Brazil iliibuka na ushindi wa mabao 5-2.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Rasunda, Pele akiwa na umri wa miaka 17 tu, alitoa mchango mkubwa kwa Brazil kutwaa ubingwa ambapo alipachika mabao mawili na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga bao katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia.

Mauzo ya jezi hiyo kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha, yameendelea kuthibitisha heshima na thamani ambayo Pele ameendelea kupewa na ulimwenguni licha ya kwamba ameshatangulia mbele za haki.

Kiasi hicho cha fedha kilichotumika kununua jezi ya Pele aliyefariki mwaka 2022, kinaifanya jezi hiyo ishike nafasi ya pili katika chati ya jezi zilizowahi kununuliwa kwa kiasi kikubwa zaidi cha fedha kulinganisha na nyingine.

Hadi sasa, jezi inayoshikilia rekodi ya kuuzwa kwa kiasi kikubwa ni ya gwiji wa zamani wa soka wa Argentina, Diego Maradona ambayo ilinunuliwa kwa Dola 9.3 milioni (Sh24.5 milioni).

Ikumbukwe Pele alitwaa Kombe la Dunia katika fainali za mashindano hayo mwaka 1958, 1962 na 1970.