Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi katika vita na rekodi ya Fontaine

MESSI Pict

Muktasari:

  • Hakupokea hata tuzo ya Golden Boot kama mfungaji bora wa mashindano hayo kwa sababu tuzo hiyo haikuwepo wakati huo. Badala yake, gazeti moja la Sweden lilimzawadia bunduki ya upepo (air rifle) kwa kumuita mpiga shabaha mahiri.

LOS ANGELES, MAREKANI: REKODI ya Just Fontaine ya kufunga mabao 13 katika Kombe la Dunia moja mwaka 1958 lililofanyika nchini Sweden ni ya kipekee. Lakini jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hakufunga mabao hayo akiwa amevaa viatu vyake mwenyewe, na wala hakutarajiwa hata kuanza katika kikosi cha kwanza cha Ufaransa.

Hakupokea hata tuzo ya Golden Boot kama mfungaji bora wa mashindano hayo kwa sababu tuzo hiyo haikuwepo wakati huo. Badala yake, gazeti moja la Sweden lilimzawadia bunduki ya upepo (air rifle) kwa kumuita mpiga shabaha mahiri.

Jina lake hutajwa kila baada ya miaka minne wakati wa Kombe la Dunia, kama kipimo cha kulinganisha wafungaji wa kizazi kipya. Hata hivyo, kwa watu wengi wa leo, Fontaine amebaki kuwa jina linaloulizwa kwenye maswali ya maarifa.

Katika Kombe la Dunia la 2026 ambapo sasa imefika hatua ya nusu fainali, Lionel Messi wa Argentina na Kylian Mbappe wa Ufaransa, wapo juu kwenye orodha ya ufungaji bora kila mmoja akifunga mabao manane.

Wawili hao wana kazi kubwa mbili, kuyasaidia mataifa yao kufuzu fainali na kwenda kubeba ubingwa, lakini pia kuifikia rekodi ya mwamba huyo na kuivunja. Hayo yote si rahisi kufanyika bila ya juhudi kubwa.

Erling Haaland wa Norway kabla ya kutolewa robo fainali, alikuwa na makali ya kucheka na nyavu akitupia saba.

Kwa nyota waliobaki, vita ya kuwania Kiatu cha Dhahabu, mbali na Messi na Mbappe, kuna wachezaji wawili wa England, Harry Kane na Jude Bellingham wenye mabao sita kila mmoja. Ingawa mashindano ya 2026 yalikuwa na timu 48 na hivyo kutoa mechi nyingi zaidi kwa washambuliaji kuongeza mabao yao, lakini bado wapo mbali na rekodi ya Fontaine ya mabao 13 aliyofunga katika mechi sita tu. Ili kufikia idadi hiyo na kuivuka, Messi na Mbappe kila mmoja anapaswa kufunga mabao sita kutoka sasa.

Tofauti na mastaa kama Pele na Maradona wanaojulikana duniani kote, Fontaine amesahaulika kwa kiasi kikubwa.

Alizaliwa Marrakesh nchini Morocco, mwezi Agosti 1933 wakati Morocco ikiwa chini ya ulinzi wa Ufaransa. Morocco ilipopata uhuru mwaka 1956, Fontaine tayari alikuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na akiichezea klabu za nchini humo, hivyo aliendelea kuitumikia timu ya taifa ya Ufaransa.

MES 01

HAKUTARAJIWA HATA KUCHEZA

Kwa mujibu wa mwanahistoria wa michezo Philip Barker, Fontaine hakuwa chaguo la kwanza la kocha.

Mshambuliaji mwingine, Rene Bliard, aliumia katika mchezo wa maandalizi, jambo lililomfungulia nafasi Fontaine dakika za mwisho.

Kutokana na mabadiliko hayo ya ghafla, Fontaine hakuwa hata na viatu vilivyomtosha. Alilazimika kuazima viatu vya mchezaji mwenzake Stephane Bruey kwa mchezo wa kwanza.

Aidha, alikuwa ametoka kufanyiwa upasuaji wa goti kabla ya mashi ndano. Ingawa hilo lilimfanya awe na mashaka ya kushiriki, pia lilimfanya afike Sweden akiwa bado ana nguvu zaidi kuliko wachezaji wengi waliokuwa wametoka kwenye msimu mrefu.

MES 02

HAKUKUWA NA PRESHA

Akizungumza na BBC mwaka 2002, Fontaine alisema: “Siku hizo hakukuwa na presha kubwa. Waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia timu walikuwa wawili tu.”

Aliendelea kusema: “Viongozi wa timu walikuwa na uhakika kwamba tungetolewa mapema, ndiyo maana walitupatia jezi tatu tu kila mmoja.”

Fontaine alisema hakuwahi kufikiria kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo.

“Hata nilikataa kupiga penalti katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.”

MES 03 (1)

NYOTA WA REIMS

Wakati huo Fontaine alikuwa akiichezea Reims, klabu iliyoshinda ubingwa na Kombe la Ufaransa msimu wa 1957-1958.

Kwa jumla alishinda mataji manne ya ligi ya Ufaransa, moja akiwa Nice na matatu akiwa Reims. Mwaka uliofuata aliiongoza Reims hadi fainali ya Kombe la Ulaya (European Cup), ingawa walipoteza dhidi ya Real Madrid. Alikuwa pia mfungaji bora wa mashindano hayo kwa mabao 10.

MES 07

USHIRIKIANO NA RAYMOND KOPA

Fontaine alikuwa na uelewano mkubwa na Raymond Kopa, ambaye baadaye alishinda Ballon d’Or ya mwaka 1958, huku Fontaine akimaliza nafasi ya tatu.

Kwa mujibu wa Barker, wawili hao walikuwa wanakaa chumba kimoja wakati wa timu ya taifa na walikuwa wakijadili sana mbinu za mchezo.


MWANZO WA MABAO

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Paraguay, Fontaine alifunga hat-trick kwenye ushindi wa mabao 7-3.

Aliendelea kufunga katika kila mechi ya Ufaransa, ikiwemo nusu fainali ambapo walifungwa 5-2 na Brazil ya Pele aliyekuwa na umri wa miaka 17.

Katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Ujerumani Magharibi, Fontaine alifunga mabao manne waliposhinda 6-3 na kufikisha jumla ya mabao 13.

MES 05

MSHAMBULIAJI WA KISASA KABLA YA WAKATI WAKE

Video za mabao yake zinaonyesha Fontaine alikuwa mshambuliaji mwenye kasi kubwa, aliyekuwa akifanya mbio za ghafla nyuma ya mabeki na kumalizia kwa utulivu.

Philip Barker anasema: “Fontaine anaonekana kama mshambuliaji wa kisasa. Alikuwa na kasi, nguvu na ujasiri.”

Bao lake la tatu dhidi ya Ujerumani lilifanana na lile maarufu la Michael Owen dhidi ya Argentina mwaka 1998, baada ya kukimbia kutoka katikati ya uwanja na kuwatoroka mabeki kabla ya kufunga.

MES 06

UFARANSA YA 1958 ILIKUWA TIMU KUBWA

Kombe la Dunia la 1958 lilikuwa na jumla ya mabao 126, idadi ya pili kubwa katika historia ya mashindano ya timu 16.

Ufaransa ilifunga mabao 23, mengi kuliko timu nyingine yoyote.

Barker anaamini kikosi hicho kinaweza kulinganishwa na timu bora za Ufaransa za mwaka 1998 na 2018.

Anasema: “Walikuwa timu ya kwanza kubwa kabisa ya Ufaransa. Washambuliaji wao watano walifunga mabao 22.”

Anasisitiza kuwa walizuiwa tu na Brazil ya mwaka 1958, ambayo ni moja ya timu bora zaidi kuwahi kutokea.

MES 08

HAKUPATA KIATU CHA DHAHABU

Kwa kuwa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot) ilianzishwa mwaka 1982, Fontaine hakuwahi kuipokea. Badala yake, mwaka 2014, FIFA ilimkabidhi Platinum Boot maalumu kwa kutambua rekodi yake ambayo haijavunjwa hadi leo.

Fontaine alisema: “Kutokuwepo kwa Golden Boot kulinisaidia. Sikuwahi kufikiria kuhusu rekodi.”

Aliendelea kusema: “Siku hizi mshambuliaji akifunga mabao matatu tu, kila mtu huanza kumuuliza kuhusu rekodi. Akianza kuifikiria, basi amekwisha.”

MES 03

KWA NINI HAKUTAMBULIKA KAMA MCHEZAJI MKUBWA ZAIDI?

Sababu kubwa ilikuwa majeraha. Mwaka 1960 alivunjika mguu katika mchezo wa ligi ya Ufaransa. Alijaribu kurejea mara kadhaa lakini majeraha yalizidi kuwa mabaya. Hatimaye alistaafu mwaka 1962 akiwa na umri wa miaka 28 tu.

Alihitimisha maisha yake ya kimataifa akiwa amech eza mechi 21 na kufunga mabao 30. Kutokana na kustaafu mapema, hakuwahi kucheza tena Kombe la Dunia.


MAISHA BAADA YA SOKA

Alisaidia kuanzisha chama cha wachezaji wa Ufaransa (UNFP) na kuwa rais wake wa kwanza.

Aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa kwa mechi mbili m

Alifundisha PSG, Toulouse na baadaye timu ya taifa ya Morocco.

Philip Barker anasema Fontaine alikuwa akifurahia kila mara watu walipokumbuka rekodi yake. Fontaine mwenyewe aliwahi kutania: “Nikifufuka baada ya miaka 200, rekodi yangu bado itakuwa ipo.” Mwamba huyo alifariki dunia Machi 1, 2023 akiwa na umri wa miaka 89.

Aliiona Ufaransa ikitwaa Kombe la Dunia mara mbili na kumshuhudia Kylian Mbappe, mmoja wa wachezaji wanaokaribia zaidi kuvunja rekodi yake, akifanya balaa uwanjani.

Barker anamalizia kwa kusema: “Ingekuwa hadithi nzuri kama Mbappe angeivunja rekodi hiyo. Lakini mabao 13 ni idadi kubwa sana. Just Fontaine ni shujaa ambaye hakupata heshima anayostahili.”