Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ivory Coast, Cameroon hakuna kutambiana

IVORY Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyokutanisha timu mbili zinazopewa nafasi ya kubeba ubingwa, Cameroon ilisawazisha bao kupitia kwa Junior Tchamadeu, ambaye shuti lake lilimbabatiza mchezaji wa Ivory Coast kabla ya kutinga nyavuni.

MARRAKECH, MOROCCO: STAA boy, Amad Diallo amefunga bao lake la pili kwenye mashindano ya Afcon 2025 wakati mabingwa watetezi Ivory Coast walipotoka sare ya 1-1 dhidi ya Cameroon katika mechi ya vuta nikuvute iliyokutanisha vigogo wa soka Afrika iliyopigwa uwanjani Marrakech.

Mechi hiyo iliyokutanisha timu mbili zinazopewa nafasi ya kubeba ubingwa, Cameroon ilisawazisha bao kupitia kwa Junior Tchamadeu, ambaye shuti lake lilimbabatiza mchezaji wa Ivory Coast kabla ya kutinga nyavuni.

Bao hilo alifunga dakika sita baada ya Amad kuifungia Tembo kwa ustadi mkubwa na hivyo kuzifanya timu hizo mbili zote kuwa na pointi zaidi zaidi ya Msumbiji kwenye Kundi F huku wakiitupa nje Gabon.

Fowadi wa Manchester United, Amad, ambaye akifunga bao pekee wakati Ivory Coast ilipoichapa Msumbiji kwenye mechi ya kwanza, alipokea pasi ya Ghislain Konan kwenye shambulizi hilo la kushtukiza na hivyo kumkwamisha mpira nyavuni huku straika wa Ufaransa, Kylian Mbappe akiwamo uwanjani hapo kushuhudia kipute hicho.

Bao hilo la Amad alifunga alilofunga kipindi cha pili lilipatikana muda mfupi baada ya bao la Franck Kessie kukataliwa kutokana na kuwapo na tukio la kuotea na Danny Namaso kugongesha mwamba.

Kipindi cha kwanza hakikuwa na hekaheka nyingi, bali kulikuwa na soka la burudani ikiwamo tukio la kugongesha mwamba lililofanywa na mchezaji Christian Kofane, ambaye ilikuwa mechi yake ya kwanza kwa Cameroon.

Timu zote nne kwenye Kundi F zitakamilisha mechi zao za tatu kwenye kundi hiyo Jumatano, ambapo Ivory Coast itakipiga na Gabon huo Marrakech na Cameroon itamalizana na Msumbiji mjini Agadir.