Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya straika, Arsenal yatua kwa Barcola

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mbali na Arsenal, huduma yake pia inawindwa na  Bayern Munich na Liverpool zilizovutiwa na kiwango alichoonyesha akiwa na PSG aliyoisaidia kuchukua ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

ARSENAL imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa, Bradley Barcola mwenye umri wa miaka 22, katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Mbali na Arsenal, huduma yake pia inawindwa na  Bayern Munich na Liverpool zilizovutiwa na kiwango alichoonyesha akiwa na PSG aliyoisaidia kuchukua ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu uliopita Barcola alicheza mechi 60 za michuano yote akafunga mabao 21 na asisti 20. Arsenal inahitaji straika ikiwa ni moja ya eneo ambalo lilikuwa na upungufu msimu uliopita na inaaminika lilichangia kutobeba ubingwa EPL. Mkataba wake unaisha 2028.


Eberechi Eze

LIVERPOOL inaitaka saini ya winga wa Crystal Palace na England mwenye umri wa miaka 26, Eberechi Eze, baada ya kuona uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Cameroon, Bryan Mbeumo ni mdogo. Mbeumo anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kujiunga na Manchester United baada ya timu hiyo kuwasilisha ofa ya zaidi ya Pauni 60 milioni mwanzoni mwa wiki hii.


Jamie Gittens

WINGA wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England, Jamie Gittens ni mmoja kati ya masupstaa wanaowindwa kwa udi na uvumba na Bayern Munich katika dirisha hili. Licha ya nia ya kutaka kumsajili, Gittens anadaiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kujiunga na Chelsea ambayo imekuwa katika mazungumzo na wawakilishi wake na Dortmund kwa muda mrefu.


Ibrahima Konate

BEKI kisiki wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa, Ibrahima Konate, 26, ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu ujao anadaiwa kukataa ofa ya Liverpool ya hivi karibuni aliyopewa ili kuongeza mkataba mpya. Inaelezwa Konate anahitaji mshahara ambao utamfanya kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa.


James Trafford

NEWCASTLE United ipo kwenye mazungumzo na Burnley ili kuipata saini ya kipa wa kimataifa wa England, James Trafford katika dirisha hili. Trafford mwenye umri wa miaka 22, huduma yake pia ilikuwa ikiwindwa na Manchester United iliyokuwa inamtaka ili akampe changamoto kipa Andre Onana ambaye ana rekodi ya kuwa na makosa mengi.


Paul Pogba

TTAARIFA ya Skysports imefichua kuwa AS Monaco bado haijafikia makubaliano na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba mwenye umri wa miaka 32, licha ya kuwapo kwa taarifa nyingine kwamba wamekubaliana. Pogba ambaye kwa sasa yupo huru amekuwa akihusishwa na timu nyingi Ulaya na nje ya bara hilo zilizoanza kumuwinda tangu alipokuwa mchezaji huru Februari, mwaka huu.


Rodrygo

REAL Madrid watataka zaidi ya pauni 77 milioni ili kumuuza winga wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 24, Rodrygo Goes, ambaye anahusishwa na uhamisho kwenda Ligi Kuu England ambako timu mbalimbali zinamtaka. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027 na Arsenal ni miongoni mwa timu zinazomtaka.


Dusan Vlahovic

JUVENTUS iko tayari kumtoa mshambuliaji wa kimataifa wa Serbia, Dusan Vlahovic, 25, na kiungo wa kimataifa wa Brazil, Douglas Luiz, mwenye umri wa miaka 27,ili kuwauza au kufanya mabadilishano na Manchester United kwa ajili ya kumsaini winga wa timu hiyo na England mwenye umri wa miaka 25, Jadon Sancho katika dirisha hili.